ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, July 19, 2014

Wazazi wa wasichana waliotekwa wakataa kukutana na Rais Jonathan

Maandamano yanafanyika kila siku kuishinikiza serikali kuwaokoa wasichana waliotekwa nyara na Boko Haram
Serikali ya Nigeria inasema familia za zaidi ya wasichana wa shule 200 waliotekwa nyara wanakataa kukutana na Rais Goodluck Jonathan kutokana na ombi la kundi la wanaharakati la Bring Back Our Girls. Tukio hilo linawaweka wasichana waliotekwa nyara kuwaingiza katika siasa za kitaifa ambapo zimepamba moto kabla ya uchaguzi mkuu mwaka ujao.

Jumatatu Rais Goodluck alimuahidi mwanaharakati Malala Yousafzai wa Pakistan anayehamasisha elimu kwa msichana kwamba atakutana na familia za wasichana walioshikiliwa mateka na wanamgambo wa kundi la Boko Haram kwa miezi mitatu iliyopita.

Mkutano ulipangwa kufanyika jumanne mjini Abuja lakini familia zimeakhirisha.

Doyin Okupe, msaidizi wa masuala ya umma kwa Rais anasema familia zimekataa kuhudhuria mkutano katika dakika za mwisho na kulilaumu Bring Back Our Girl, kundi moja la wanaharakati ambalo linafanya maandamano takribani kila siku kudai kuokolewa kwa wasichana hao.

Hata hivyo bwana Okupe analishutumu kundi la Bring Back Our Girls kwa kushirikiana na wanasiasa wa upinzani wanaotaka kuchukua nafasi ya bwana Jonathan katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.

Serikali inashutumu kampeni za Bring Back Our Girls kwa mchezo mchafu na wenye kuchukiza na kurudia ahadi ya serikali ya kuwatafuta wasichana na kutokomeza uasi wa kundi la Boko Haram.

VOA

No comments: