Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni
Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe akipokelewa kwa shangwe na Viongozi
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Kata ya Kipara-Mtua, Wilaya ya Nachingwea
mkoani Lindi kabla ya kuzungumza nao kuhusu masuala mbalimbali ya maendeleo ya
Jimbo na kujua kero mbalimbali zinazowakabili viongozi hao. Aidha, Waziri
Chikawe aliwataka viongozi hao kuwa na umoja ili kukipa nguvu chama chao hasa katika
kipindi hiki wanapoelekea katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni
Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe akikitunza kikundi cha kwaya cha
CCM Kata ya Kipara-Mtua baada ya kutumbuiza katika mkutano wake na Viongozi wa
Kata hiyo iliyopo Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi. Waziri Chikawe aliwataka
viongozi hao kuwa na umoja ili kukipa nguvu chama chao hasa katika kipindi hiki
wanapoelekea katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni
Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe akizungumza na Viongozi wa Chama
Cha Mapinduzi (CCM) wa Kata ya Kipara-Mtua, Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi.
Waziri Chikawe aliwataka viongozi hao kuwa na umoja ili kukipa nguvu chama chao
hasa katika kipindi hiki wanapoelekea katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni
Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (meza kuu katikati) akimsikiliza
kwa makini Mkandarasi wa Wakala wa Umeme Vijijini (REA), Rabinarayan Bishoyi (kulia)
wakati alipokuwa anatoa maelezo kwa viongozi wa CCM Kata ya Mtua (hawapo
pichani). Kwa mujibu wa Mkandarasi huyo, tayari ameanza kuweka nguzo za umeme
kutoka Nachingwea mjini kwenda vijiji vya Namatula, Kihuwe, Naipingo,
Mapwechero, Farm 15, Kipara Mtua, Jiungeni na Mtua ambapo vijijini hivyo
vinatarajiwa kupata umeme hivi karibuni.
Kushoto ni Meneja wa Shirika la Umeme Tanesco, Josiah Hegeleize ambaye
Shirika lake linashirikiana na REA kuleta umeme katika vijiji hivyo.
Shekhe Mkuu wa Wilaya
ya Nachingwea, Abdul Mpakate akimshukuru Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (kushoto hajavaa
kofia), kwa kuandaa futari maalum kwa Waumini wa Dini ya Kiislamu wa Msikiti
Mkuu wa Nachingwea, mkoani Lindi. Waziri Chikawe aliandaa futari hiyo kwa ajili
ya kutoa sadaka kwa waumini hao katika kipindi hiki cha mfungo wa Mwezi Mtukufu
wa Ramadhan.
Picha zote na Felix
Mwagara.
2 comments:
Mheshimiwa CHIKAWE tuache kudanganyana miaka hamsini na ushehe juu!! Hilo jingo unalotolea mazungumzo unaona ni sawa kabisa kwa chama kikubwa cha wizi namna hii ya CCM yaani bora hata hilo joho ulilovaa wewe!! tuacheni utani viongozi wa TZ.
Jamani hii nayo ni Aibu Waziri mkubwa inabidi utengeneze kwenu Dooo.
Post a Comment