ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, July 8, 2014

WAZIRI WA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA ATEMBELEA BANDA LA JESHI LA MAGEREZA MAONESHO YA 38 YA BIASHARA YA KIMATAIFA JIJINI, DAR ES SALAAM

 Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mhe. Christopher Chiza(Shati jeupe) akiangalia zao la Mahindi yaliyolimwa katika Bustani Maalum ya Shamba Darasa katika Banda la Jeshi la Magereza alipotembelea Banda hilo kujionea Kilimo cha Kisasa na Biashara Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa, Jijini Dar es Salaam(wa kwanza kulia) ni Mtaalam wa Kilimo wa Jeshi la Magereza, Mrakibu wa Magereza, Uswege Mwakahesya.
 Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mhe. Christopher Chiza akiangalia zao la Kitunguu kinachozalishwa na Jeshi la Magereza katika Gereza Mang'ola Mkoani Arusha alipotembelea Banda la Jeshi la Magereza, Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa, Jijini Dar es Salaam. Mhe. Waziri Chiza ameahidi kushirikiana na Jeshi la Magereza katika kutafuta fursa ya Masoko ya ndani na nje ya nchi(wa pili kulia ni Afisa Masoko wa Shirika la Magereza, Mrakibu Msaidizi wa Magereza, Yunge Saganda.
 Muonekano wa Bustani ya Shamba Darasa katika Banda la Jeshi la Magereza lililopo katika Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ambapo sehemu kubwa ya Wananchi wananufaika na Elimu ya Kilimo cha Kisasa na chenye tija katika Maonesho hayo yanayoendelea Jijini, Dar es Salaam.
 Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mhe. Christopher Chiza akiondoka katika Banda la Jeshi la Magereza alipotembelea Banda hilo Julai 7, 2014 katika Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea Jijini, Dar es Salaam.
Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mhe. Christopher Chiza(Shati jeupe) akifanya mahojiano na Mwandishi wa Habari baada ya kutembelea Bustani Maalum ya Shamba Darasa ya Jeshi la Magereza iliyopo katika Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa, Jijini Dar es Salaam. Katika Mahojiano hayo Mhe. Waziri ameahidi Kushirikiana na Jeshi la Magereza katika kutoa elimu ya Kilimo Bora kwa Wakulima hapa Nchini pamoja na kulisaidia Jeshi hilo ili kupata fursa mbalimbali ya kupata Wawekezaji wa ndani na nje ya nchi katika masuala ya Kilimo.

1 comment:

Anonymous said...

Amakweli nchi yetu ni ndogo, huwezi kuamini ndani ya wiki 2 serikali yote imeishia viwanja vya Sabasaba..