Picha ikionyesha jinsi maj i yenye kemikali yanavyotiririshwa toka katika kiwanda cha
kutengeneza nguo cha NIDA kilichopo barabara ya Mandela.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira Injinia
Dkt Binilith Mahenge akiangalia uharibifu wa mazingira uliosababishwa na maji yenye kemikali
yanayotiririshwa na kiwanda cha NIDA. Anayemfuatia ni Mkurugenzi Mtendaji wa
NEMC Bonaventura Baya, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Eng. Angelina
Madete.
Jengo la kiwanda cha NIDA likionekana kwa nje
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira Injinia
Dkt Binilith Mahenge akiongea na Menejimenti ya kiwanda cha kutengeneza nguo
cha NIDA Textiles kuhu kiwanda hicho kinavyoharibu mazingira kwa kutiririsha
maji yenye kemikali katika mto kibangu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira Injinia
Dkt Binilith Mahenge, akiongea na Vyombo vya habari kuhusu ziara yake
aliyoifanya katika kiwanda cha NIDA textiles jijini Dar es Salaam
Rai imetolewa kwa wawekezaji wote Nchini kuhakikisha
wanajali na kutunza Mazingira.Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na Waziri wa
Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt Binilith Mahenge wakati alipofanya ziara ya kutembelea kiwanda cha
kutengeneza nguo cha NIDA kilichopo barabara ya Mandela katika kata ya Kigogo
jijini Dar es Saalam.
Kiwanda hicho ambacho kinalalamikiwa na wananchi kuwa
kinatiririsha maji machafu yenye kemikali katika mto kibangu uliopo pembeni ya
kiwanda hiko ambako wananchi wanalima mbogamboga kando yamto huo na wanatumia
kula pia wanauza ili kujipatia kipato
pasipo kujali athari zilizopo kwenye maji hayo yenye kemikali.
Akiongea na Menejimenti ya kiwanda hiko Dkt. Mahenge baada
ya kutemebelea mto huo na kujionea maji yalivyoathiriwa na kemikali zitokazo
kiwandani, aliitaka Menejimenti ya kiwanda hiko kuacha mara moja kutiririsha
maji yenye kemikali katika mto kibangu na hivyo basi kuchukua hatua za
kitaalamu ili kuondoa kemikali zilizopo kwenye maji hayo.
Akiongea kwa niaba ya Menejimenti ya Kiwanda Afisa Utawala
Mohammed Olewo aliahidi kwamba watafanyia kazi maagizo ya Waziri kwa ufasaha na
wanaahidi watarekebisha makosa yote yaliyotokea pia watadumisha na kutunza mazingira.
Ziara hiyo ni moja ya ziara za Waziri anazofanya
kutembelea maeneo mbalimbali ya jiji la
Dar es Salaam kwa ajili ya kukagua utunzaji wa mazingira.
No comments:
Post a Comment