ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, August 2, 2014

19 kortini kwa ugaidi

Baadhi ya ndugu wa watuhumiwa wa ugaidi wakiwa nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha wakati ndugu zao wakirejeshwa mahabusu jana. Picha na Filbert Rweyemamu

Arusha. Watu 19 wamefikishwa mahakamani jana kwa mashtaka tofauti ikiwemo kushawishi, kufadhili na kutekeleza ugaidi kwenye matukio kadhaa yaliyotokea jijini Arusha.
Washtakiwa 12 kati ya hao pia wanakabiliwa na tuhuma za kuua na kujaribu kuua kwenye tukio la mlipuko wa bomu uliotokea kwenye mkutano wa kampeni wa Chadema Juni 15, mwaka jana.
Wakisomewa mashtaka na jopo la mawakili wa Serikali Felix Kwetukwao, Augutino Kombe na Maricelino Mwamunyange, washtakiwa hao walidaiwa kutenda makosa hayo kati ya Oktoba 25, 2012 hadi Julai 21, mwaka huu.
Mbele ya Hakimu Mkazi Devotha Msofe, watuhumiwa hao hawakutakiwa kujibu lolote kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka kisheria ya kusikiliza mashauri yanayowakabili na wote wamerejeshwa mahabusu hadi Agosti 15, mwaka huu shauri lao litakapotajwa.
Waliofikishwa mahakamani jana ni Yusuph Huta (30), Abdul Humud (30), Jafari Lema (38), Said Temba (42), Kassim Ramadhan (34), Ramadhan Waziri (28), Abashar Omar (24), Abdulrahman Hassan (41), Niganya Hamisi (28), Morris Muzi (44), Baraka Bilango (40) na Hassan Omar (40). 
Walioshtakiwa kwa tukio la mlipuko wa bomu Arusha uliotokea nyumbani kwa aliyekuwa Katibu wa Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata), Mkoa wa Arusha, Abdulkarim Jonjo, Oktoba 25, mwaka 2012, ni Yusuph Huta (30), Kassim Ramadhan (34), Mustapha Kiagho (49) na Abdul-Aziz Mohamed (49).
Jaffar Lema (38), Yusuph Huta (30) na wenzao 10 wanatuhumiwa kuhusika kwenye tukio la mlipuko wa bomu kwenye Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, eneo la Olasiti Mei 5, mwaka jana.
Watuhumiwa ni Ramadhan Waziri (28), Abdul Humud (30), Said Temba (42), Kassim Ramadhan (34), Abdulrahaman Hassan (41), Morris Muzi (44), Niganya Hamisi (28), Baraka Bilango (40), Hassan Omar (40) na Hassan Mfinanga wanadaiwa kuwamwagia tindikali Sheikh Said Juma Makamba wa Msikiti wa Kwa Morombo na Sheikh Mustapha Khiago wa Msikiti Mkuu wa Ijumaa jijini Arusha.
Jaffar Lema (38) na Ibrahim Lenard (37) pia wanadaiwa kuhusika na tukio la bomu lililolipuka Baa ya Arusha Night Park Aprili 13, mwaka huu. Watu 16 tayari wamefikishwa mahakamani kuhusiana na mlipuko huo.
Watuhumiwa wengine waliofikishwa mahakamani jana ni Yahaya Twahir (37), Idd Yusuph (23), Said Temba (42), Anwar Hayel (29), Jafar Lema (38), Hassan Mfinanga (57), Yusuph Ramadhan (23) Abashar Omar (24), Yusuph Huta (30), Sumaiya Ally (19), Abashar Omar (24), Kimoro Mchana (25), Hassan Omar (25), Morris Muzi (44), Niganya Hamis Niganya (28) na Baraka Bolango (40).
Watuhumiwa Ibrahim Leonard (37), Anwar Hayel (29) na Yasin Shaban (20) walifikishwa mahakamani kwa tuhuma za kuhamasisha vitendo vya kigaidi kupitia mitandao ya kijamii.
MWANANCHI

No comments: