Mazungumzo yakiendelea baina yake na mgeni wake.
Mhe. Mjenga akiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni wake, Bw. Ammar Saeb, Mkurugenzi wa Jumeirah Emirates Towers Hotel.
Balozi Mdogo wa Tanzania, Dubai, Mhe. Omar Mjenga, leo amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi mpya wa Jumeirah Emirates Towers Hotel Bw. Ammar Saeb.
Katika mazungumzo yao, wamejadiliana kuhusu mpango wa kuutangaza utalii wa Tanzania, Dubai. Hivyo basi, Mhe. Mjenga ameuomba uongozi wa JET kugharamia malazi ya siku tatu kwa wajumbe 20 kutoka kampuni 20 za utalii kutoka Tanzania (20 top tour and travel companies) kuja dubai kuonana na wenzao kwa ajili ya kubalishana mawazo na maarifa kuhusu kuvutia utalii wa nchi zote mbili.
Shirika la ndege la Emirates, lilishakubali hapo awali kugharamia tiketi 20 kwa wajumbe wa kampuni kutoka Tanzania.
Ubalozi Mdogo unafanya mawasiliano na Wizara ya Maliasili na Utalii, pamoja na Bodi ya Utalii ya Tanzania (TTB) ili kupata kampuni kubwa 20 kutoka Tanzania.
Aidha, Ubalozi Mdogo upo mbioni kuandaa mkutano wa uwekezaji kwenye sekta ya utalii hapo Novemba mwaka huu, baada ya kuandaa kwa ufanisi mkubwa, mkutano kama huo wa uwekezaji kwenye sekta ya nyumba, uliofanyika Juni 11, 2014 na kufunguliwa rasmi na Mhe. Dk. Mohamed Bilal, Makamu wa Rais wa JMT.
No comments:
Post a Comment