Bondia Thomas Mashali katikati akisaini mkataba wa kucheza na Henry Wandera kutoka Kenya Novemba 4 katika ukumbi wa New Madiba 'Korini' uliopo Tandale Dar es salaam wanaoshudia kushoto ni Raisi wa oganaizesheni ya ngumi za kulipwa nchini TPBO, Yassini Abdallah 'Ostadhi' na promota wa mpambano huo Khamis Ally
Rais wa TPBO Yassin Abdala akiandika mkataba wa bondia Thomas Mashali katikati atakaepambana na mkenya Henry Wandera Novemba 4 katika ukumbi wa New Madiba 'Korini' uliopo Tandale Dar es salaam kulia ni promota wa mpambano huo Khamis Ally
Bondia Thomas Mashali katikati akisaini mkataba wa kucheza na Henry Wandera kutoka Kenya Novemba 4 katika ukumbi wa New Madiba 'Korini' uliopo Tandale Dar es salaam wanaoshudia kushoto ni Raisi wa oganaizesheni ya ngumi za kulipwa nchini TPBO, Yassini Abdallah 'Ostadhi' na promota wa mpambano huo Khamis Ally picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com
BONDIA Thomas Mashali 'Simba asiyefugika' anatarajia kupanda uringoni tena novemba 4 mwaka huu kumvaa mkenya Henry Wandera mpambano utakaofanyika katika ukumbi wa New Madiba zamani Korini
Mashali anapigana uku akiwa na historia ya kupoteza mpambano wake wa mwisho zidi ya bondia Mada Maugo ambapo walicheza katika uwanja wa taifa na kupoteza kwa point mpambano huo
akizungumzia mpambano huo Mashali amesema atokubali kupoteza tena mchezo huuo ukizingatia anachezea nyumbani kwao alopozaliwa na ndipo alipoanzia ngumi maeneo ya Tandale hivyo sito kubali niaibike mbele ya ndugu zangu hivyo nawambia wapenzi waje kwa wingi kuangalia mashali anavyofanya kazi yake ya mchezo wa masumbwi
nae promota wa mpambano huo Khamis Ally amewahakikishia kuwa sehemu ya parkingi ni kubwa na ulinzi ni wa kutosha kifupi katika ulinzi tumejipanga vizuri pia siku hiyo kutakuwa na mapambano mengine mazuri ya utangulizi ambapo mabondia wengi wamejitokeza kucheza siku hiyo
siku hiyo pia kutakuwa na huuzwaji wa
DVD ambazo zinatoa mwanga kwa mchezaji kujua mchezo na kufahamu zaidi mbinu mpya zitumiwazo na mataifa mbali mbali Duniani.
Wakiwemo mabondia bingwa wa dunia kama Manny Paquaio,Floyd Maywether,Amir Khani, Mohamed Ali ,Mike Tayson na wengine wengi wanaotamba na waliotamba katika mchezo huo wa masumbwi Duniani
kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' ametoa wito kwa makampuni mbalimbali kujitokeza kutoa sapoti ya mchezo wa masumbwi kwani ndio mchezo pekee unaoweza kututoa kimasomaso watanzania tukafurahi
No comments:
Post a Comment