ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, August 14, 2014

CECAFA:KCCA ya Uganda yatinga robo fainali

KCCA imechapa Atletico ya Burundi goli 1 bila,goli lililotiwa kimiani na Alan Omony
Timu ya KCCA ya Uganda imekuwa timu nyingine iliyojihakikishia tiketi ya kusonga mbele katika robo fainali ya mashindano ya vilabu bingwa afrika mashariki na kati maarufu kombe la Kagame.

KCCA imechapa Atletico ya Burundi goli 1 bila,goli lililotiwa kimiani na mshambuliaji Alan Omony kwa njia ya penalty kunako dakika ya 32 ya mchezo.

Atletico ambao wana alama tatu wamebaki na mechi moja dhidi ya Telecom kuamua nafasi ya tatu ya kusonga mbele.

Mechi nyingine ya kundi hilo,timu ya APR ya Rwanda nayo imefuzu katika robo fainali kufwatia ushindi wake wa goli 1 bila dhidi ya timu dhaifu ya Telecom ya Djibuti,mechi iliyopigwa kwenye uwanja wa Nyamirambo jijini Kigali.

Goli la kwanza lilipatikana kunako dakika ya 37 mfungaji akiwa ni mlinzi Emery Bayisenge.

Kazi haikuwa rahisi kama ilivyotarajiwa na wengi kwani goli hilo lilikaa hadi mwisho wa mchezo lakini likatosha APR kuandika alama tatu.

Mechi zitakazopigwa alhamisi, KMKM watatakiwa kufanya kazi ya ziada kuwafunga wenyeji Rayon Sport ikiwa wanataka kufuzu katika hatua ya robo fainali, vinginevyo watakuwa wa kwanza kuyaaga mashindano haya.

Rayon Sports wao watahitaji sare yoyote ili kuwa miongoni mwa timu tatu zitakazofuzu.

Katika kundi hilo pia,kunatarajiwa mechi kali kati ya Atlabara ya Sudani kusini na Adama City ya Ethiopia kwa mushindi atafuzu moja kwa moja katika hatua ijayo.

Mechi nyingine itapigwa kati ya Polisi ya Rwanda iliyokwishakata tiketi yake ikitarajiwa kufunga kazi dhidi ya Banadar ya Somalia.

BBC

No comments: