Advertisements

Friday, August 22, 2014

CRISTIANO RONALDO AOMBA UONGOZI WA RAEL MADRID WASIMUUZE DI MARIA

Default
Imeripotiwa kuwa mchezaji Cristiano Ronaldo na mwenzie Sergio Ramos wanajaribu kuongea na Rais wa Real Florentino Perez abadilishe uamuzi wake wa kumuuza mchezaji Di Maria kwa Manchester United wakati huu wa kiangazi.

Kocha wa timu hiyo Carlo Ancelotti amethibitisha tayari mazungumuzo ya awali yameishafanyika na sababu za kumuuza mchezaji huyo ni kutokana na usajili wa wachezaji wawili waliosajiliwa na timu hiyo msimu huu ambao ni  Toni Kroos na James Rodriguez inawezekana Di Maria akauzwa kwa paundi milioni 50.

No comments: