Ile movie ya kwanza ya kimataifa kutoka Tanzania sasa inapatikana kupitia mtandao wa iTunes : bit.ly/goingbongoitunes. Going Bongo imekuwa filamu ya kwanza ya Africa Mashariki kukubalika na Apple kwa kuwa na viwango vya juu, vilivyowekwa katika filamu hiyo. Hadi sasa ni filamu chache za Afrika kwa ujumla ambazo zimekubaliwa kuwekwa iTunes.
DVD ya filamu hiyo pia inapatikana hapa: bit.ly/goingbongodvd
Going Bongo inahusu daktari wa Marekani ambaye anakuja bila hiyari yake kufanya kazi Tanzania.
Filamu hiyo imefanyika 75% Dar-es-salaam na 25% Los Angeles. Waigizaji wa filamu hiyo wametoka nchi za Tanzania, Marekani, Italy, Kenya, Uingereza na nyinginezo.
Baadhi ya waigizaji kutoka Tanzania ni Ernest Napoleon (zamani Channel5/EATV), Evance Bukuku (Choice FM), Sauda Kilumanga (ITV, Egoli na nyinginezo), Ahmed Ulotu "Mzee Chilo"(Sumu ya Mapenzi, Cross My Sin ), McDonald Haule (Siri ya Mtungi, The Team).
Hapa chini ni trailer ya filamu hiyo. Hongera kwenu Going Bongo!
Unaweza kuwasiliana na watengenezaji wa filamu hiyo kupitia Facebook
Going Bongo Movie Trailer from Going Bongo on Vimeo.
No comments:
Post a Comment