ANGALIA LIVE NEWS

Monday, August 25, 2014

KAMPUNI YA MSAMA PROMOTION NA JESHI LA POLISI WAKAMATA KAZI FEKI ZA WASANII‏

1
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion, Alex Msama, akizungumza na waandishi wa habari kwenye kituo cha polisi cha Urafiki wakati akitangaza kukamatwa kwa watuhumiwa 17 kwa kurudufu kazi za wasanii kinyume na utaratibu yaani kazi feki katika jiji la Dar es Salaam na baadhi ya mikoa ambapo kazi feki za wasanii zilizokamatwa thamani yake ni shilingi milioni 12, Kulia ni ASP Denis Moyo mkuu wa upelelezi wa kituo hicho ambaye amesema amethibitisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao ambao wanasubiri kupelekwa mahakamani.
2
Alex Msama na Denis Moyo wakionyesha CD feki zilizokamatwa jijini Dar es Salaam.

3
Msama akionyesha mashine ya Photocopy inayotumiwa kurudufu CD hizo.
4
Msama na Denis Moyo wakionyesha CD feki zilizokamatwa.
5
Msama akifafanua zaidi kuhusu wizi huo.
6
Kituo cha polisi cha Urafiki.
(PICHA NA FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)

No comments: