Advertisements

Friday, August 22, 2014

KATIBU MKUU KIONGOZI OMBENI SEFUE AWAAGA WANAFUNZI WA TANZANIA WALIOPATA UFADHILI WA MASOMO NCHINI UHOLANZI

Makamu Mkuu wa Misheni ya Uholanzi, Bi. Hinke Nanta (kushoto) akijadiliana jambo na Katibu Mkuu Kiongozi (katikati) wakati wa hafla ya kuwaaga wanafunzi hao iliyofanyika 21 Agosti, 2014 nyumbani kwa Balozi eneo la Oysterbay Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Kiongozi Ombeni Sefue akitoa nasaha zake kwa wanafunzi (watanzania) waliopata udhamini kamili wa masomo nchini Uholanzi wakati wa hafla ya kuwaaga wanafunzi hao iliyofanyika 21 Agosti, 2014 nyumbani kwa Balozi eneo la Oysterbay Jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania, Mhe. Jaap Frederiks akitoa hotuba yake kwa wanafunzi (watanzania) waliopata udhamini kamili wa masomo nchini Uholanzi wakati wa hafla ya kuwaaga wanafunzi hao iliyofanyika 21 Agosti, 2014 nyumbani kwa Balozi eneo la Oysterbay Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanafunzi waliopata udhamini kamili wa masomo nchini Uholanzi wakisikiliza kwa makini hotuba toka kwa mgeni rasmi Katibu Mkuu Kiongozi Ombeni Sefue wakati wa hafla ya kuwaaga wanafunzi hao iliyofanyika 21 Agosti, 2014 nyumbani kwa Balozi eneo la Oysterbay Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanafunzi waliopata udhamini kamili wa masomo nchini Uholanzi wakisikiliza kwa makini hotuba toka kwa mgeni rasmi Katibu Mkuu Kiongozi Ombeni Sefue wakati wa hafla ya kuwaaga wanafunzi hao iliyofanyika 21 Agosti, 2014 nyumbani kwa Balozi eneo la Oysterbay Jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi wakitanzania waliopata udhamini kamili wa masomo katika vyuo mbalimbali nchini Uholanzi wakifurahi kwa pamoja wakiwa na wageni wegine waalikwa pamoja na mgeni rasmi wakati wa hafla ya kuwaaga wanafunzi hao iliyofanyika 21 Agosti, 2014 nyumbani kwa Balozi eneo la Oysterbay Jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi wakitanzania waliopata udhamini kamili wa masomo katika vyuo mbalimbali nchini Uholanzi wakifurahi kwa pamoja wakiwa na wageni wegine waalikwa pamoja na mgeni rasmi wakati wa hafla ya kuwaaga wanafunzi hao iliyofanyika 21 Agosti, 2014 nyumbani kwa Balozi eneo la Oysterbay Jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi wakitanzania waliopata udhamini kamili wa masomo katika vyuo mbalimbali nchini Uholanzi wakifurahi kwa pamoja wakiwa na wageni wegine waalikwa pamoja na mgeni rasmi wakati wa hafla ya kuwaaga wanafunzi hao iliyofanyika 21 Agosti, 2014 nyumbani kwa Balozi eneo la Oysterbay Jijini Dar es Salaam.Picha zote na Benedict Liwenga-MAELEZO-DSM

Na Benedict Liwenga-MAELEZO
KATIBU Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue amehudhuria hafla ya kuwaaga wanafunzi waliopata udhamini kwenda kusoma nchini Uholanzi katika sekta mbalimbali zikiwemo za mafuta na gesi, miundombinu, kilimo, maji, afya pamoja na Maendeleo ya sekta binafsi.
Hafla hiyo ilifanyika nyumbani kwa Balozi wa Uholanzi eneo la Oysterbay Jijini Dar es salaam ambapo Katibu Kiongozi ndiye alikuwa mgeni rasmi wa hafla hiyo.
Katibu Kiongozi amesema kuwa kuna umuhimu mkubwa sana wa program ilianzishwa na nchi ya Uholanzi wa kuwasaidia watanzania kupata ufadhili kamili wa kwenda kusoma masomo mbalimbali nchini humo na ujuzi wanaoupata uweze kulisaidia Taifa pamoja na watanzania wengine kwa ujumla.
“Ninaamini kuwa wanafunzi hawa waliopata ufadhili huu wa masomo mbalimbali nchini Uholanzi watapata fursa kubwa ya kusomea mambo mbalimbali na ujuzi huu hawatakaa nao wenyewe binafsi, bali watalisaidia taifa na watanzania wengine, hivyo wajenge moyo huo wa kutokuwa wabinafsi”. Alisema Sefue.
Naye Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania, Mhe. Jaap Frederiks amesema kuwa amefurahi kwa muamko mkubwa wa watanzania wengi wa kuomba nafasi za masomo nchini kwake na amewaasa wengine kuiga mfano huo kwani nchi yake itaendelea na programu hiyo kulingana na bajeti pamoja na wataalam waliopo nchini Uholanzi.
“Nchi yangu inatoa fursa ya masomo kwa watanzania kwenda kusoma lakini tunaangalia maeneo ambayo tuna wataalam ambao wanaweza kuwasaidia watanzania kuwapa elimu, hivyo ni jukumu lao wenyewe watanzania kuaamua maeneo gani ya kusomea pamoja na kozi wazipendezo”. Alisema Frederiks

Katika kipindi cha miaka Hamsini iliyopita, zaidi ya watanzania Elfu tano wamepata udhamini wa kusoma katika sekta mbalimbali zikiwemo Utawala wa Fedha, Uhandisi, Miundombinu, Kilimo, Afya, Elimu na Utawala ambapo hii inaifanya Tanzania kuwa moja ya ya wanufaikaji wakubwa duniani wa programu hii ya udhamini wa masomo, ambapo wengi wa watanzania waliopata nafasi hizi wameshika nyazifa muhimu katika Jamii ya Tanzania kitu ambacho kinaendeleza ukuaji wa uchumi wa Tanzania.

No comments: