Advertisements

Friday, August 22, 2014

KIKAO CHA BARAZA LA UVCCM MKOA WA ARUSHA CHAKUTANA KUMJADILI NAIBU KATIBU UVCCM MKOA

Mwenyekiti UVCCM mkoa wa Arusha Robinson Meitinyiku akitoa taarifa ya ufafanuzi kwa waandishi wa habari juu ya taarifa za upotoshaji zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari na baadhi ya viongozi wa UVCCM mkoani hapa. Ambao Mkutano huo ulitanguliwa na Kikao cha Baraza la UVCCM Mkoa wa Arusha waliaofikiana kutoa maamuzi juu ya mgogoro wao na Kaimu Katibu wa UVCCM Mkoa wa Arusha Gerald Mwadalu anayetuhumiwa kufunga ofisi na matumizi mabaya ya fedha za umoja huo.
Katibu wa UVCCM wilaya ya Karatu Ally Rajabu akisoma maazimio ya Kikao cha Baraza la UVCCM Mkoa wa Arusha lililokutana leo na kutoa maazimio 17 likiwamo la kumpiga marufuku Kaimu Katibu UVCCM Mkoa wa Arusha Gerald Mwadalu asijihusishe na kazi za UVCCM mkoa wa Arusha.
Mwenyekiti wa UCVVM Mkoa wa Arusha Robnson Meitinyiku na baadhi ya wajumbe wa Baraza la UVCCM Mkoa wa Arusha wakisikiliza maazimio yaliyopitishwa na wajumbe wakati yalipokuwa yakisomwa mbele ya waandishi wa habari mjini hapa
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa UVCCM Mkoa wa Arusha Diwani Kimayi katikatika pamoja na wajumbe wenzake wakisikiliza maazimio yaliyokuwa yakisomwa ambapo kwa upande wake alitoa ushauri kwa Baraza Kuu la Taifa la UVCCM kwamba linapoteua watendaji lie linaangalia watendaji wenye sifa.
Sehemu ya mkutano wa waandishi wa habari na wajumbe wa Kikao cha Baraza la UVCCM mkoa wa Arusha kikiendelea leo katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Rose
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatulia maazimio yaliyofikiwa na Kikao cha Baraza la UVCCM Mkoa wa Arusha kilichofanyika leo jioni.Ambapo Baraza hilo liliazimia kuanza kufanyiak kwa ukaguzi wa mara kwa mara katika ofisi za UVCCM mkoa kwa kila mwezi kwa ajili ya kdhibiti ubadhilifu.
Baadhi ya wajumbe wa Kikao cha Baraza la UVCCM Mkoa wa Arusha wakifuatilia kwa makini ajenda za kikao hicho, ambapo Baraza hilo lililaani kitendo cha Kaimu Katibu wa UVCCM Mkoa cha kufunga ofisi ili Kamati ya Utekelezaji isifanye kikao ambacho walikubaliana pia kitendo cha kukwepa kuitisha vikao licha ya kukubaliana na Mwenyekiti kama kanuni inavyotaka na kuuotosha umma kwamba Kamati ya Utekelezaji ndio iliyofunga ofisi.
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa Robson Meitinyiku akifuatilia kikao cha Baraza la UVCCM Mkoa wa Arusha kilichofanyika leo jijini hapa na kupitia maazimio ya kumtaka Katibu wa CCMM Mkao Mary Chatanda asiingilie Jumuiya hiyo bali awe mshauri kupitia bvikao vya jumuiya ambapo yeye ni Mjumbe katika vikao vya Utekelezaji na vya Baraza
Baadhi ya wajumbe wa Kikao cha Baraza la UVCCM Mkoa wa Arusha wakifuatilia maazimio yaliyokuwa yakisomwa mbele ya wanahabari leo mjini hapa ambapo Baraza hili liliazimia kwamba endao Katibu wa Mkoa Mary Chatanda atabainika kuwa na ubadhilifu basi asihamishwe mkoa mwingine na apelekwe mahakamani ili iwe fundisho. Jamii Blog

No comments: