Advertisements

Thursday, August 21, 2014

KITUO CHA RADIO CHA NCHINI MAREKANI WKYS KUANZA KUPIGA NYIMBO KUTOKA AFRIKA

Dj Joe Cat Daddy
Kituo cha Radio nchini Marekani WKYS kilichopo Washington DC kitaanza rasmi kuanzia kesho Ijumaa Aug 22, 2014 kupiga nyimbo za kiafrika. Akiongea na Vijimambo dj  Joe Cat Daddy Mtanzania anayefanyakazi kwenye radio hiyo maarufu kwa upigaji wa nyimbo za hip hop amesema ameishapata baraka kwa wakuu wake wa kazi kwamba anaweza kuanza kupiga nyimbo kutoka Afrika. Dj Joe alliendelea kusema hiki kipindi kitakua kinarushwa kila siku ya Ijumaa usiku kuanzia saa 5 kamili usiku kwa saa ET ambapo Tanzania itakua ni alfajiri kuamkia Jumamosi. Dj Joe aliomba wnamuziki wa Tanzania kama wana nyimbo zinazofanya vizuri katika anga ya muziki Tanzania na kwingeneko kuitumia nafasi hii. Email yake ni djjoe202@gmail.com
 na unaweza kuisikiliza WKYS kwenye mtandao kwa kubofya hapa

1 comment:

Anonymous said...

Congratulations, you were on instrgram all day being mentioned initially by Iamduro about the new Chuck Brown song in collab with King Kanja. Our own TZian DJ on WKYS!!!!!! How international is DC?