ANGALIA LIVE NEWS

Monday, August 18, 2014

Libe its time to let it GO! Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni.

WanaDMV wakipiga kura

Kwenye mashindano yoyote lazima kuna atakae shinda na atakae shindwa.Kama wote tulivyoshuhudia kwenye huu uchaguzi wa Rais DMV.Iddi ndo ameibuka mshindi.Japo kuwa kulikuwa na makosa kidogo lakini pia tumeshuhudia Kamati ilivyo sahihisha kihalali.Sasa kwa nini wewe mwenzetu Libe unakuwa mgumu kukubali matokeo.Ujue kuwa huwatendei haki watu waliokuchagua kwa kuwaacha wagae gae kwa kutokumkubali Rais alieshinda.Itafika siku hata waliokupigia kura watakukimbia kutokana na wewe kuwa hivyo.Na hata Uchaguzi ukirudiwa sidhani kama utapata kura nyingi kama ulizozipata mara ya kwanza.Kwa sababu wengi watakuwa wamekujua kuwa wewe ni mtu mng’ang’anizi na usiekubali kitu hata kama kipo sawa.

     Mtu unaweza leta mabadiliko na maendeleo katika jamii wakati wowote na ukiwa popote.Sio lazima uwe kiongozi ndio u make difference.Libe,unaweza fanya kazi na Iddi kama ulivyotuahidi kwenye campaign ili kuleta maendeleo DMV, na hata kwengineko.Na kama ukiona kuna ugumu wa kufanya nae kazi basi pia unaweza saidia jamii kivyako vyako,mbona mifano ipo mingi tunaiona.Ukikubali haya matokeo utakuwa sio tu umeonyesha mfano mzuri hivi sasa, bali hata huko mbeleni itakusaidia na watu watakuona kama ni mtu unaefaa.


     Hizo Pesa mlizochanga sijui za wakili au za nini.Ingekuwa vyema mngesaidia ndugu zetu Muhimbili wanaohitaji/subiri Damu na matibabu mengineyo.Au hata kusaidia mayatima tulionao nyumbani ambao wanahitaji vitu muhimu katika maisha (necessities).Na vile vile ingekuwa vyema kama ndugu Iddi nae akibadilika kwa kupunguza minuso ya mara kwa mara, ambayo inagharimiwa na Jumuiya.Ni bora kuzitumia hizo pesa kufanya mambo ya maana, Mfano hata kuwanunulia health insurance ndugu wa baadhi ya wana DMV ambayo na hakika wana familia nyumbani Tanzania ambao hawana health insurance.Kwa vile wewe mwenyewe Rais una ujuzi wa ku verify Income kutokana na kazi yako ili kujua nani ana qualify ambae hana uwezo mkubwa kifedha,basi wasaidie wenzio kwenye mambo ya maana kama hayo.Just USD 300 per year ukimlipia mtu mmoja au zaidi utakuwa umefanya jambo la maana sana.

Ni mimi mpenda haki.
Buhite Jabry.
08/17/2014

11 comments:

Anonymous said...

Unaakili sana unampa ushauri wa maana ,mungu akubariki kwa mawazo mazuri.

Anonymous said...

Libe usiwasikilize hawa ignorant mimi nimekupigia kura na ninataka usimame kidete kwenye justice.wapenda haki WOTE hawaogopi mkono wa sheria,libe hana baya alilofanya zaidi ya kwenda kwenye sheria sheria sheria.sasa hawa wapambe wa idd wanaogopa sheria kwa vile judge atakapoamua kesi hii hamjuwi idd wala libe ataamua base na facts kitu ambacho bodi ya uchaguzi hakikufanya .team idd wengi hawakusoma wababuruzwa na wamezoea mizizo na mupasho saa zote time hiyo hatuna tena.TUACHE SHERIA ICHUKUWE MKONDO WAKE.THIS IS AMERICA
ASANTE.

Anonymous said...

Hii ni uwongo mwingine mimi buhite jabry sikuandika hiyo massage hapo juu,kuna mtu kaandika halafu kaweka jina langu dj luke naomba uiyondoe haraka

Anonymous said...

Wewe huna msimamo njaa inakusumbuwa,kwanza ulikuwa mamluki rudi tu team idd usilete fitna zako

Anonymous said...

kwa idadi ya wapiga kura na waliohudhuria nyama choma inabidi tujiulize maswali mengi hii. Inabidi uchaguzi huru uitishwe na Libe na Sandaly wasiwe wagombea, period!

Anonymous said...

Umesema ukweli kabisa, Kusaidia Community sio mpaka uwe kiongozi but again Libe sio mtu wa hayo mambo.Libe ameanza kuoneka kwenye community kwasababu ya uchaguzi na the reason ya kugombea ni binafsi na sio ya kusaidia watu kama anavyosema ni sababu apate platform ya kujulikana ili kugombea ubenge Tanzania.Good luck ya kugombea Madawaska Tz watakumaliza, siku mbili tuu na, Jazba lako. Jazba si Uongozi, please reserch on how to be a great Leader

Anonymous said...

Uchaguzi urudiwe na Sandaly na Libe wasiruhusiwe kugombea, period! mwenyekiti kusema uchaguzi ni VOID halafu next day wanatangaza mshindi kuna kitu nyuma ya pazia na wana DMV hatutaki kuburuzwa

Anonymous said...

Wewe dada ulimpigia debe sana Libe na kumu'ondozi na kumpa kura yako na kumsaliti RAIS Iddy sandale,sasa Leo imekuwaje unamshauri akubali matokeo badala ya kumchangia hiyo Hela ya kwenda kortini, wakati muheshimiwa Libe bado ana uchu na uongozi.Libe kaza Kamba usikate tamaa!!

Anonymous said...

Buhite unampinzani wewe kiboko sasa ukweli ndio huo batalogoto benyewe dada thx

Anonymous said...

I thought kazi ya urais ni volunteer work, how are you going to sue some one kwa sababu umeshindwa ku volunteer.Libe must have his own individual agenda, you can still serve DMV community without being a president and hujaonyesha leadership at all baada ya uchaguzi.You still have a loong way to go to become a leader.I hope you will lear from this..do the right thing bring people together.Nilikuvotia now unaniangusha.

Anonymous said...

he is not going to let it go, uchaguzi huu umejaaa zulma ya hali ya juu.
libe don't let it go man fight for your right wameshazoea sana hawa kujifanyia mambo yao kienyeji enyeji na kishikaji kishikaji na bila maendeleo kwa wana jamii ya kitanzania.