madaktari wakitoa huduma dhidi ya Ebola
Shirika la Madaktari wasio na mipaka Medecins Sans Frontiers wametahadharisha kuhusu wizara ya afya nchini Liberia kuzidiwa nguvu na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola katika eneo la Afrika Magharibi.
Mratibu wa mambo ya dharura wa shirika hilo nchini humo amesema serikali haikutilia maanani vya kutosha madhara ambgayo yangesababishwa na ugonjwa huo na kwamba mfumo wa afya kwa sasa upo katika hali ya kushindwa.
Nchini Siera Lione, majeshi yameweka vizuizi katika maeneo yaliyoathirika na ugonjwa huo.
Raia wa Uingereza ambaye ni mfanya biashara katika eneo la Kanema kaskazini mwa nchini hiyo anaeleza madhara wanayopata kutokana vizuizi vya zilivyowekwa.
Credit:BBC
No comments:
Post a Comment