ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, August 26, 2014

MANCHESTER UNITED WAGEUZWA KICHWA CHA MWENDA WAZIMU UPITIE UBAO HAPO CHINI

Manchester United walipoteana kabisa katika mchezo huu licha ya kuto wachezesha wachezaji wao maalufu lakini hicho hakiwezi kuwa kisinginzio cha kufungwa goli 4 na timu hii yenye kushiriki ligi ya ligi 1. MK Dons kwenye msimamo wa ligi yao inashika nafasi ya 7 katika timu 24.
Giggs kocha msaidizi akiwa haamini kinachotokea hadi anaamua kuzuia uso wake kwa mkono kama ishara ya masikitiko na huku kocha mkuu akijaribu kuandika kama tasmini ya mchezo kwa wachezaji wake. Kocha mkuu wa Manchester Van Gaal huu ni mchezo wake wa tatu kwenye mbio za mataji ndani ya Uingereza na hajashida hata mchezo mmoja amepoteza mchezo mmoja na draw moja kwenye BPL na huu ni mchezo wapili kupoteza lakini hii ni katika kulisaka kombe la Capital One Cup. Capital One Cup ni mashindani yanayoshirikisha timu za madaraja ya chini zenye wachezaji wenye vipaji wanaosaka nafasi ya kuonekana na kucheza kwenye BPL.
Mwiba ambao hawatausahau Manchester United Benik Afoba akishangilia bao lake la nne kati ya mawili aliyofunga katika mchezo huo. Afoba ni kinda alietokea katika kikosi cha Wenger na kumtoa kwa mkopo kwa MK Dons kiroho safi  hili aongeze maujuzi .
Huyu nae anaitwa Grigg alitupia mabao mawili sawa na Afoba.
Sura za majonzi wote hawaamini kinachotokea
Huyo ndiyo Afobe ni sheeeeeeeeda!!!! akimchambua golikipa wa Manchester United De Gea kama Ubuyu yake rangi vile ukiumung'unya tu mweupeee!!

No comments: