Advertisements

Thursday, August 21, 2014

Marekani Kuwasaka Wauaji wa Forley

Kitengo cha sheria nchini ya Marekani kimeanza kufanya uchunguzi wa jinai dhidi ya kifo chamwandishi wa habari mwenye asili ya Marekani ,James Foley aliyeuawa na wapiganaji wa kiislamu wenye msimamo mkali.

Mwanasheria mkuu wa kitengo hicho,Eric Holder ameweka wazi kuwa wote waliohusika na mauaji ya mwandishi huo watawatia mkononi muda si mrefu.

Maofisa wa serikali ya Marekani wandai kwamba askari hao wauaji walidai kiasi kikubwa cha pesa zipatazo dola za kimarekani zaidi ya milioni mia moja na thelathini kama fidia ya kumuachilia James Foley.

Marekani imekwisha anza harakati za kuwasaka na hatimaye kuwakamata waliohusika na mauaji ya mwandishi huyo kwa kurusha ndege zake takriban sita katika anga inayomilikiwa na waislamu kaskazini mwa Iraq.

pamoja na kwamba waislam hao kutishia kumuua mmarekani mwingine wanayemshikilia kama ulipizaji wa kisasi endapo mashambulio yataelemea upande wao. BBC

1 comment:

Anonymous said...

What a horrible way to die! May his soul rest in peace.. Amen