Advertisements

Thursday, August 21, 2014

Liverpool yamnyakua Mario Balotelli-BBC

Klabu ya Liverpool imemsajili mshambuliaji machachari Mario Balotelli kwa paundi milioni 16.

Kocha wa Liverpool Brendan Rodgers amesema kuwa wameamua kumchukua mshambuliaji huyo ili kuziba pengo lililoachwa wazi na Luis Suarez ambaye amehamia Barcelona.

Balotelli ambaye mwaka jana alijiunga na timu ya AC millan kwa uhamisho wa paund milion 19 akitokea Machester City hadi sasa ameweza kufunga magoli 30 katika michezo 54.

Balotelli alijiunga na Manchester City August 2010 kwa paundi milion 24 wakati huo akitokea Inter Milan ambako aliiwezesha klabu yake kuchukua kombe katika michuano ya ligiya England.

No comments: