ANGALIA LIVE NEWS

Friday, August 15, 2014

Mgombea kiti cha rais Brazil afariki katika ajali ya ndege-VOA

Marehemu Eduardo Campos akifanya kampeni Aug. 6, 2014  mjini Brasilia, Brazil.
Mgombea kiti cha rais Eduardo Campos na baadhi ya wafanyakazi wa kampeni yake wafariki wakati ndege yao binafsi kuanguka katika mji wa pwani wa Santos, ikitokea Rio de Jeneiro.

Ajali ya ndege nchini Brazil ambayo ilimwua mgombea urais wa chama cha kisoshialisti,Eduardo Campos na wafanyakazi wake sita imesababisha ratiba ya uchaguzi wa urais iliyopangwa Oktoba tano kuingia matatani.

Campos na wafanyakazi kadhaa kwenye kampeni yake walikufa wakati ndege yao binafsi iliyokuwa ikisafiri kutoka Rio de Janeiro ikielekea pwani ya mji wa Santos kupata ajali wakati ikijaribu kutua kukiwa na hali mbaya ya hewa.

Wachambuzi wa kisiasa wanasema mgombea mwenza wa Campos, waziri wa zamani wa mazingira Marina Silva, anaweza kuingia kwenye kinyang’anyiro hicho katika muda wa siku 10 zijazo kwa mujibu wa sheria za Brazil.

No comments: