Wakiwa katika mazungumzo
Katika mazungumzo yao, Mhe. Mjenga amewaomba kuangalia uwezekano wa kuajiri Watanzania kwenye Benki hiyo kuja kufanya kazi hapa Dubai. Mwaka jana, UBL ilifungua ofisi zake Dar es salaam.
Mhe. Mjenga amewaomba pia kuifanya ofisi ya Dar es salaam kuwa ofisi ya Kanda ya Afrika. Aidha, wamegusia suala la kufungua matawi zaidi Arusha, Moshi, mwanza, mbeya na matawi mengine zaidi Jijini Dar es salaam.
Hii yote itafanikisha kuongeza nafadi za ajira kwa Watanzania
Mhe. Mjenga, Balozi Mdogo wa Tanzania, Dubai akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wakuu wa benki ya UBL ya Dubai. Kulia mwa Mhe. Mjenga ni Bw. Shaikh Muhammad Liaque, Makamu wa Rais wa UBL na kushoto ni Bw. Syed Abbas Bokhari
No comments:
Post a Comment