ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, August 13, 2014

Mo Farah azimia akifanya mazoezi

Mwanariadha maarufu wa Uingereza Mo Farah alikimbizwa hospitalini baada ya kuzimia wakati akifanya mazoezi.

Bingwa huyo wa Olimpiki wa mbio za mita 5,000 na 10,000, ambaye atashiriki mashindano yatakayofanyika mjini Zurich wiki hii, anasema kuwa tukio hilo lilimlazimisha kukosa mashindano ya jumuiya ya madola yaliyofanyika mjini Gllasgow.

"niling'olewa jino lakini tangu hapo nikaanza kuugua.Nilikuwa nafanya mazoezi wakati nilipozirai,'' asema Faram mwenye umri wa miaka 31.

"nilikuwa nahisi uchungu mwingi sana tumboni mwangu. Nililazimika kukimbizwa hospitalini kwa ndege.''

Walidhani kwamba Moyo wangu ulikuwa na tatizo la kiafya wala sivyo. ''

Farah alihitaji kupewa matibabu ya dharura baada ya kuzirai alipokuwa anashiriki mbio za Marathon mjini London mwezi Machi. Alisema alishtuka sana kufuatia tukio hilo.

"nilikuwa na simu yangu mfukoni , nilipoamuka nikampigia simu mwenzanu ambaye tunfanya mazoezi naye, alinisaidia na kuiweka kitandani,'' alisema Mo

"hali ilikuwa mbaya sana. Nililazwa hospitalini kwa siku nne.''

Sikuwa na mtu wa kunisadia wakati nilipoanguka . Nilikuwa peke yangu. Tuliamua ikiwa ilikuwa lazima kusafirisha mke wangu na watoto kwa ndege.

"tangu hapo nimekuwa nikihisi uchungu mwingi, hiki ni kama kichekesho. Na hapo ndopo walidhani kuwa Moyo wangu ilikuwa na tatizo.

Lakini baada ya matibu ilibainika kwamba Mo hakuwa na tatizo lolote na Moyo wake.

BBC

No comments: