ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, August 26, 2014

RAIS KIKWETE AZINDUA BARABARA YA DUMILA-RUDEWA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Mussa Iyombe pamoja na Makamu mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa barabara ya Dumila-Rudewa yenye urefu wa Kilomita 45 iliyojengwa kwa kiwango cha lami.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifungua jiwe la msingi kuashiria ufunguzi rasmi wa Dumila-Rudewa yenye urefu wa Kilomita 45 iliyojengwa kwa kiwango cha lami.
Sehemu ya barabara ya Dumila-Rudewa yenye urefu wa Kilomita 45 iliyojengwa kwa kiwango cha lami.

Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na baadhi ya Watendaji kutoka Wizara ya Ujenzi ambao walikuwa wakisubiri tukio la ufunguzi wa barabara ya Dumila-Rudewa yenye urefu wa Kilomita 45 uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Mussa Iyombe kushoto akiwa pamoja na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS Mhandisi Patrick Mfugale wakitazama ramani pamoja na picha mbalimbali za barabara ya Dumila-Rudewa yenye urefu wa Kilomita 45 iliyojengwa kwa kiwango cha lami.
Mc Mavunde kulia akiwatambulisha watendaji mbalimbali kutoka Wizara ya ujenzi kabla ya Ufunguzi rasmi wa barabara ya Dumila-Rudewa
Sehemu ya wakazi wa Dumila waliojitokeza kwa wingi wakimsiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete licha ya giza kuingia mjini Dumila.

No comments: