Waziri wa Habari Utamaduni, Utalii na Michezo Saidi Ali Mbarouk (wakatikati) katika ziara ya kutembelea mabaa na mahoteli ya kitalii, kutokana na wananchi kulalamikia vitendo vya upigwaji wa ngoma na vitendo viovu, (kulia) Mkuu wa Wilaya Kaskani (B) Unguja Khamis Jabir Makame na kushoto ni Sheha wa Kiwengwa Bw. Maulid Masudi Ame huko Kiwengwa.
Waziri wa Habari Utamaduni, Utalii na Michezo Saidi Ali Mbarouk na Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini B, Khamis Jabir Makame wakipata maelezo kutoka kwa mmiliki wa Baa ya Vision Pub Francis Vicoguga juu ya undeshaji wa kazi zake katika Baa hiyo.
Waziri wa Habari Utamaduni, Utalii na Michezo Saidi Ali Mbarouk,akizungumza na wananchi na wamiliki wa mahoteli na baa katika kijiji cha Kiwengwa mara baada ya ziara yake ya kutembelea hoteli hizo.
Mratibu wa Wanawake na Watoto Bi Mtumwa Rashid Khalifa, mkazi wa Kiwengwa akizungumzia kero wanazozipata kutokana upigwaji wa madisko katika mabaa kijijini hapo.(Picha na Jamila Abdalla – Maelezo Zanzibar)
Waziri wa Habari,Utamaduni , Utalii na Michezo Saidi Ali Mbaruok amepiga marufuku shughuli zote za upigaji wa disko katika eneo la Kiwengwa mpaka pale Serikali ya wilaya itapotoa maelekezo maalumu ya upigaji wa disko hilo kwa utaratibu unaofaa.
Agizo hilo amelitoa huko Kiwengwa Mkoa wa kaskazini “A”wilaya ya kaskazini B Unguja katika Ofisi ya umoja wa maendeleo wa kijiji cha kiwengwa wakati alipokuwa akifanya mazungumzo na wamiliki wa mabaa mikahawa,na kumbi na starehe juu ya kukithiri wa upigaji wa magoma kucha.
Amesema amelazimika kuzifunga shughuli zote za upigaji wa madisko usiku kutokana na kutokua na utaratibu mzuri wa upigaji ngoma hizo usiku hali ambayo inapelekea wageni wa kitalii na wenyeji kuchukia hali hiyo kwa kukosa usingizi na kusumbuliwa wagonjwa wenye shindikizo la damu.
Amsema hali hiyo haiwezekani kuona inaendelea katika hali kama hiyo kwani inapoteza muelekeo na mstakabali mwema wanchi na raia kwaujumla.
“Nimepokea messsege ya kwamba watalii wamefika kusema wanaondoka na kutafutiwa sehemu nyengine wakapunzike kutokana na zogo kuwa jingi la madisko,hili hiliwezekani liendelee”lisema Waziri.
Aidha alisema haiwezekani kuona utamaduni wa burudani unavurugwa kituambacho ni kosa kufanya hivyo na kwenda kinyume na taratibuzao selka zao.
“Kuazia leo napiga marufuku mpaka sheha wa shehia hii aridhie hata kama kuna kibali ,kwani sheha yeye ndio anae jua hali za raia wake kuna wagonja,na wenyemaradhi ya kuhitaji kupumzika hatutaki kuona masuala yasio na utaratibu.”aliongeza Waziri.
“Mimi kazi yangu ni kuutangaza utalii na sio utalii uharibiwe ,tufahamu kua ulalii Zanzibar ndio uchumi unao tegemewa kwa sasa kwa hivyo tulinde,”aliongeza Waziri Said.
Hata hivyo waziri huyo alichukia vitendo vya uwasharati vilivyo tapakaa katika kijiji hicho na kujenga mabaa karibu na nyumba za ibada kitu ambacho aliagiza kwa mkuu wa wilaya kuyafanyia kazi.
Nao wazazi wa kiwengwa Othumani mnyanja na mtumwa Rashidi walisema kiwengwa hivisasa imepoteza muelekeo kwani watoto wao wanaishia katika madisko na kukosa masoma kitiambacho ni hatari kwao.
Aidha walisema kua watoto wao wakiwa na umri mdogo na kujishughulisha na masuala ya kimapezi jambo linalo wafanya nialama ya kupotea na kuacha mila za kislamu.
Wakitaja maeneo ya nayopigwa miziki na watoto wao kwenda ni pamoja na maeneo yanayo pigwa madisko hayo ni pamoja na ,kigorofani, vishani wazalendo pub, Kamili View,Obama Baa na kigorofani eneo la mafarasi.
Nae miliki wa ukumbi wa Disko wa PERUU B, Peruce Osward Buhoma akiulizwa swali na waziri kwanini anafanya mazogo usiku alikiri kwa kusema hufanya hivyo kwaajili ya kuvuta wateja na kufanya ushindani kila mmoja kwa ajili ya kusikika zaidi kuliko mweziwe.
Bibi huyo na wezake walisema wanaweza kujirekebisha lakini pawe na utaratibu wa kupiga madisko kwa zamu na utaratubu mzuri utakao wekwa na uongozi
1 comment:
afadhali amethubutu
Post a Comment