ANGALIA LIVE NEWS

Monday, August 25, 2014

TAIFA LETU

AGIZO RASMI KWA VYAMA VYA SIASA KUTOKA KWA WATANZANIA:


ELIMU BORA, UCHUMI BORA NA AJIRA BORA KWA WATANZANIA WOTE

Taifa letu ni tajiri kwenye madini, mafuta, gesi na mazao mbalimbali na lina uwezo mkubwa wa kujenga na kuimarisha elimu bora kwa wote, uchumi bora na ajira kwa wote. Elimu yetu ni duni, uchumi wetu ni kwa wachache na ajira hazitoshelezi. Hivi Taifa letu litaendelea kuwa masikini mpaka lini?

Watanzania tuna haki, tunawajibika na tunataka kujenga nchi yetu katika misingi ya elimu bora kwa wote, uchumi bora kwa wote na ajira kwa wote. Miaka 50 baada ya uhuru, umaskini wetu si dhihaka bali ni dhambi mbele ya Mwenyezi Mungu.

Uchaguzi ujao hatutachagua chama bali tutamchagua mgombea mwenye sifa ya kuthamini elimu bora kwa wote, uchumi bora kwa wote na ajira kwa wote.. Mgombea lazima awe muelewa kuwa Taifa letu linahitaji elimu kwanza kwa wakulima, kwa wafanyabiashara, kwa wafanyakazi; uchumi bora na ajira kwa wote. Taifa letu linahitaji kiongozi si mwenye uwezo tu bali aliyeonyesha uwezo kwa vitendo si kwa maneno.

Maagizo ya watanzania kwa vyama vya siasa ni kwamba, awamu hii tuleteeni mgombea mwenye kuthamini elimu bora, uchumi bora na ajira, kwa wote. Tunataka mgombea mwenye kuelewa kuwa Serikali ina wajibu wa kutimiza matakwa haya na yeye yuko tayari kuongoza, kusimamia na kutekeleza bila kutetereka au kuyumbishwa yumbishwa.

Watanzania tutalinda, tutatetea na kudumisha amani na upendo katika Taifa letu.

TUSIKILIZE NA ZINGATA, WATANZANIA TUNA KIU YA MAENDELEO.

Tutaendelea na mjadala huu kila wiki.

No comments: