Ni masaa 24 yamepita toka uchaguzi ufanyike huku Tume ya Uchaguzi bado imekuwa na kigugumizi kutoa msimamo na kutangaza matokeo. Uchaguzi huu uliofanyika August 9, 2014 umedhihirika pasi na shaka kuwa ni BATILI. Baadhi ya mambo yanayofanya uchaguzi huu ni batili na “Team Libe for DMV President 2014” inaweka wazi msimamo wake kuwa, HATUTAKUBALI MATOKEO YEYOTE YATAKAYO TOLEWA NA TUME KWA SASA KWANI UCHAGUZI HUU NI BATILI “FRAUD ELECTION”.
Baadhi ya sababu zinazo batilisha uchaguzi huu ni kama zifuatazo;
Moja, jumla ya watu walio piga kura ilikuwa 430 huku Idd Sandaly alipata jumla ya kura 231 na Liberatus kura 214. Ukijumlisha kura za Liberatus na Idd unapata kura 445, yaani kura maruhani ni 15 (214+231=445). Hii ina maanisha kuwa, Liberatus alipata 49.76% na Idd alipata 53.72% ya kura zilizo pigwa. Ukijumrisha hizi asilimia unapata 103.48% (53.72+49.79= 103.48%). Hii ni bila kuweka “absentee ballot. Ukiweka absentee ballot Liberatus ana kura 222 ambayo ni 51.62% ya kura zilizo pigwa na Idd ana 235 ambayo ni 54.65% ya kura zilizo pigwa. Hii ina maanisha ukijumrisha jumla ya asilimia za Idd na Liberatus unapata 106.27% (51.62%+54.65%). Hii haileti maana yeyote kama wagombea wote wana kura zaidi ya asilimi 50% ya zilizopigwa; UCHAGUZI HUU NI BATILI.
Pili, baada ya mkanganyiko huu kutokea, wakala wa Liberatus hakuyakubali matokeo na wala hakuweka sahihi. Aliomba kura zihesabiwe tena; alikataliwa. Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi baada ya kuona mkanganyiko huu alitamka kuwa uchaguzi huu ni “VOID” na hawezi kumtangaza mshindi. Mzee Safari alishinikizwa na baadhi ya watu wa Board of Trustee akiwepo Ulotu, baadhi ya watu wa Tume ya
Uchaguzi na mashabiki wa Idd Sandaly atangaze matokeo. Mzee Safari alisema hatotangaza matokeo na kama mnataka kutangaza; chukueni mic hii hapa. Baada ya mtafaruku huu, Mwenyekiti wa Board of Trustee, Hamza Mwamoyo, alimuita Mzee Safari faragha. Baada ya Mzee Safari kurudi alisema “sitatangaza mshindi bali nitatangaza numbers”. Hadi leo hii Jumapil, August 10, 2014, 9pm hakuna mshindi aliyetangazwa wala Tume haijatoa neno. UCHAGUZI HUU NI BATILI.
Uchaguzi na mashabiki wa Idd Sandaly atangaze matokeo. Mzee Safari alisema hatotangaza matokeo na kama mnataka kutangaza; chukueni mic hii hapa. Baada ya mtafaruku huu, Mwenyekiti wa Board of Trustee, Hamza Mwamoyo, alimuita Mzee Safari faragha. Baada ya Mzee Safari kurudi alisema “sitatangaza mshindi bali nitatangaza numbers”. Hadi leo hii Jumapil, August 10, 2014, 9pm hakuna mshindi aliyetangazwa wala Tume haijatoa neno. UCHAGUZI HUU NI BATILI.
Tatu, mwenyekiti wa Board of Trustee, Hamza Mwamoyo, alizichukua kura zote akimuahidi wakala wa Liberatus kuwa tutafanya “re-count” na akamuagiza amwambie Liberatus anipigie simu ili tuone tutafanya vipi “re-count”. Liberatus alimpigia simu Hamza Mwamoyo zaidi ya mara tano bila majibu. Mzee Mwamoyo alitokomea na kura zile kusiko julikana. Hadi walaka huu unaandikwa baada ya masaa 24; Ndg Hamza Mwamoyo hajarejesha simu ya Liberatus. Swali la kimsingi ni kuwa; inakuaje kura za makatibu zilifanyiwa “re-count” na gap yake ilikuwa kubwa kuliko kura za marais na za marais zikataliwe kufanyiwa re-count? UCHAGUZI HUU NI BATILI
Nne, watu waliopiga kura walikuwa 430, kura za makamu wa Rais zilikuwa kama ifuatavyo; Heriet Shangarai kura 333 na mama Salma Moshi kura 94. Ukijumrisha hizi kura unapata jumla ya 427 (333+94). Matokeo haya bado yapo chini ya jumla ya watu waliopiga kura 430 (let say kura 3 ziliharibika). Wakati kura za maraisi jumla yake ilikuwa 445; je kura 15 zilitokea wapi? Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi, Asha Nyang’anyi, amekili kuwa kuna kura ziliharibika na wala hakusema ni ngapi. Alisema nyingi. Baada ya kumbana sana aliendelea kusema nyingi bila kuwa “specific” ni kura ngapi ziliharibika. Hata kama kuna kura nyingi zilizo haribika; bado zitakuwa zinaenda nje ya kura halali 430.
Kura za katibu zilikuwa kama ifuatavyo; Said Mwamende alipata kura 251 na Ismail Mwilima alipata kura 171. Ukijumrisha kura hizi unapata jumla ya 422 (251+171). Bado kura za makatibu zipo chini ya jumla ya wapiga kura walio tokea 430; hii inamaana kura 8 ziliharibika. Je, ni kwa nini za marais zilizidi kura 430 hadi kufikia kura 445? Kura 15 zilitokea wapi?. Makamu wa katibu Bernadeta Kaiza alipata kura 254 na Solomn Cris alipata kura 167; jumla ya kura hizi ni 421 (254+167). Bado na hizi zipo chini ya jumla ya watu walio kuja 430; hii inamaana kura 9 ziliharibika. Kwa nini za maraisi zinazidi watu walio kuja? UCHAGUZI HUU NI BATILI
Tano, Ndg. Idd Sandaly amekuwa akijitangaza kuwa yeye ni mshindi na leo hii jumapili August 10, 2014 alikuwa kwenye mkutano wa CCM akijitangaza kuwa yeye ni Rais wa DMV. Je, Idd amejuaje kuwa yeye ni Rais mpya wa DMV ilihali Tume bado haijatangaza mshindi?
Kwa hoja hizi tajwa “Team Libe for DMV Community President 2014” inapenda kuchukua fursa hii kuutangazia Umma wa DMV na wapenzi wake 222 yaani 51.62% ya wapiga kura kuwa: HATUTA TAMBUA MATOKEO YEYOTE YATAKAYO TANGAZWA NA TUME JUU YA UCHAGUZI HUU BATILI. “Team Libe for DMV Community President 2014” bado inaamini Board na Tume ya Uchaguzi watatumia busara kutatua mgogoro huu ili tuwe na jumuia isiyo na mpasuko. Pia, wahusika watambue kuwa; Team Libe ina watu zaidi ya 222 (51.6% ya walio piga kura 430) ambao wanahitaji kupewa majibu stahiki. Ustawi wa jumuia upo mikonpni mwa Tume ya Uchaguzi. Nawahasa watu wa Team Libe for DMV president wawe na uvumilivu huku tukisubiri kauli ya Tume ya Uchaguzi.
Imetolewa August 10, 2014
Mwanaid Love “Mona”/ Campaign Manager
UNITED WE STAND; DIVIDED WE FALL
2 comments:
jamani kubalini yaishe ilimfanye kazi pamoja sasa kweli mtafanya hiyo kazi kamamlivyosema mkishindwa mtamsapoti mshindi mbona majungu DC hayaishi.
Ndiko kiwanda kilipo Weweee!!
Post a Comment