Advertisements

Wednesday, August 20, 2014

TIMU YA AZAM FC YAFA KIUME YATOLEWA KWA MATUTA 4-3


Timu ya Azam FC wawakilishi pekee wa Tanzania katika mashindano ya klabu bingwa afrika mashariki imetolewa leo katika robo fainali ya pili kwa kufungwa na El Marreikh ya Sudani kwa magoli ya matuta baada ya timu hizo kumaliza dadika za kawaida bila kufungana. 

Beki Shomary Kapombe na mshambuliajiLionel Saint- Preux kutoka Haiti ndio waliokosa penati Wachezaji ambao walielezwa awali kuwa wanasumbuliwa na vyama za paja lakini wakashuka katika dimba la Nyamirambo mjini Kigali Rwanda licha ya mlinda mlango Mwadin Ally kufanya kazi nzuri ya kupangua penati ya wapinzani wao.

No comments: