*WANAFUNZI WA VYUO WAMO
*WALIOHAMA DMV KUHAMIA MAJIMBO MENGINE WARUDI KUPIGA KURA
Na Mwandishi wetu, DMVUchaguzi wa Jumuiya ya Watanzania DMV kufanyika kesho siku ya Jumamosi Aug 9, 2014 GLEMONT LOCAL PARK iliyopo Wheaton Maryland, nchini Marekani. Tofauti na miaka iliyopita uchaguzi wa mwaka huu umekua na kampeni za aina yake zilizokua na mvuto wa aina yake na kufanya Watanzania wengine kote Duniani kuufuatilia kwa karibu zaidi kutokana na wagombea kujinadi kwa staili ya pekee ambayo haijawahi tokea tangia chaguzi hizi za DMV ziliponza kufanyika tangia miaka 80.
Chaguzi ya safari hii imepigwa kampeni ya nguvu hasa kwa wagombea wa Urais Bwn. Liberatus Mwang'ombe na Rais wa sasa anayegombea kwa mara ya pili, Bwn. Iddi Sandaly. Katika kampeni zao kumetokea malumbano ya hapa na pale hasa katika maswala ya kutofautiana kwa hoja na kujibizana kwenye mitandao kitu kilichogeuza sura mpya ya kampeni hizi na kuziteka roho za Watanzania wengine kote Duniani na kuwafanya kuatilia uchaguzi huu kwa karibu zaidi. Wagombea wengine katika kinyang'anyiro hiki ni Harriet Shangarai na Salma Moshi wanaogombea makamu wa Rais, Ismail Mwilima na Said Mwamende wanaogombea Ukatibu. Bernadeta Kaiza na Solomon Chris makamu Ukatibu na mweka hazina ni Jasmine Rubama ambaye hana mpinzani.
Mambo mengi yamejitokeza katika uchaguzi huu yakiwemo watu wengine kuweka kura zao wazi za nani watakayempigia kura. Jambo lingine lililoweka historia ni Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula nae atatumia haki yake ya msingi kama mwanDMV kupiga kura kitu ambcho hakijawahi fanywa na Balozi yeyote tangia Jumuiya hii ya Watanzania DMV ilipoanzishwa. Jambo lingine ambalo ni geni katika uchaguzi huu ni wagombea kwenda vyuoni kutafuta wanafunzi wanaosoma DMV na kujinadi huko na katika majina yaliyotolewa na kamati ya uchaguzi yamo majina ya wanavyuo Watanzania wanaosoma vyuo vya DMV kitu ambacho hakijawahi tokea miaka ya nyuma. Jambo lingine ambalo limejitokeza katika uchaguzi huu ni Watanzania ambao walishahama DMV miaka ya nyuma lakini kutokana na bado wanatumia vitambulisho vya DMV wameamua kurudi kupiga kura kuwachagua wagombea wao. Jambo lingine ni wagombea wengine kufungua mitandao kwenye facebook kwa ajili ya kupigia kampeni zao na kuwa vikundi vya SMS kwenye whatsup kwa ajili ya kampezi za vikundi vyao akiwemo mgombea Liberatus Mwang'ombe pamoja nakuwa na vitu hivyo pia amefungua blog yake inayoendesha maswala yote ya kampeni zake.
Hayo ndio mambo kadhaa yaliyojitokeza katika uchaguzi huu unaoandika historia mpya kwa wakaazi wa DMV. Milango ya ukumbi itafunguliwa kuanzia saa 8 mchana (2pm) mpaka saa 4 usiku (10 pm) na Watanzania wa DMV wametakiwa kufika na vitambulisho vyao pia kamati ya uchaguzi imetoa majina ya wapiga kura na wameomba Wana DMV wayapitie na waangalie kama ulilipia na jina lako halipo wanaomba uwapatie taarifa pia wameomba kama unashaka na jina lololete au mapungufu tafadhali waandikie email- uchaguzi2014@gmail.com hii ni katika kuhakikisha uchaguzi unakuwa wa haki na unaofuata misingi ya katiba.
No comments:
Post a Comment