ANGALIA LIVE NEWS

Friday, August 22, 2014

Viongozi wa Uamsho wadai polisi waliwafanyia ukatili

Wanachama wa kundi la uamsho wanaotuhumiwa kujihusisha na vitendo vya ugaidi wakitoka wakiwa chini ya ulinzi wa Magereza walipofikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam jana. Picha na Venance Nestory

Dar es Salaam. Viongozi wa Jumuiya za Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (Jumiki), akiwamo Sheikh Farid Hadi Ahmed (43) wameilalamikia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa polisi “walitumia ushenzi na ukatili” wakati wa kuwahoji.
Farid na washtakiwa wenzake wanakabiliwa na mashtaka manne likiwamo la kuwaingiza watu nchini kushiriki katika vitendo vya ugaidi, kusaidia na kuwezesha kufanyika vitendo hivyo.
Washtakiwa hao walitoa malalamiko hayo jana kwa Hakimu Mkazi, Hellen Liwa muda mfupi baada ya Wakili wa Serikali, Peter Njike kuiomba Mahakama iwaruhusu washtakiwa saba kwenda polisi kuhojiwa kwa ajili ya upelelezi zaidi.
Baada ya wakili huyo kuwasilisha ombi hilo, Sheikh Farid aliuliza: “Wametuomba tena kwenda kuhojiwa? Kwanza waliotuhoji hawakutumia ustaarabu wala ubinadamu ilikuwa ni ushenzi na ukatili. Walituhoji wakati tukiwa watupu na kutupiga”.
Sheikh Farid alidai kuwa kiongozi Mkuu wa Jumuiya za Uamsho, Sheikh Mselem Ali Mselem alimweleza watu hao walichomfanyia.
Hata hivyo, Hakimu Liwa alimwambia alimtaka kuzungumzia kile ambacho amekiona siyo cha kusimuliwa.
Aliendelea kueleza: “Walipigwa na wala hawakupewa matibabu na watu wameumizwa, utakuta wanakojoa damu wiki moja hadi mbili, tunaomba wafanyiwe uchunguzi wa afya zao.”
Mshtakiwa Salum Ali aliiomba Mahakama kupeleka daktari mahabusu kwa madai kuwa wanafanyiwa vitendo vya ‘kuingiliwa kinguvu’ na kuhoji kwa nini wamekamatwa Zanzibar na kushtakiwa Bara wakati waliokamatwa Arusha walishtakiwa hukohuko na hawakupelekwa Dar es Salaam au Zanzibar?
Akiendelea kutoa malalamiko yake, Sheikh Farid alidai kuwa wao wamekamatwa kwa sababu hawautaki Muungano na kwamba huo ndiyo msingi wa kesi hiyo.
Baada ya kauli hiyo, Hakimu Liwa alisema: “Tupo kwenye mchakato wa Katiba Mpya na masuala ya muungano yanatajwa mbona watu wanasema na hawakamatwi?”
Mara baada ya Hakimu Liwa kusema hayo, Sheikh Farid alidai ni kwa sababu wao wanahubiri ukweli na watu wanaukubali.
Hakimu Liwa aliiahirisha kesi hiyo hadi Septemba 3, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa na kuangalia kama upelelezi utakuwa umekamilika au la.
Katika kesi hiyo, Sheikh Farid na Jamal Nooridin Swalehe (38) waliunganishwa na wenzao 18 mahakamani hapo.
Mbali na Sheikh Farid na Jamal, washtakiwa wengine wanaokabiliwa na mashtaka hayo ni Nassoro Hamad, Hassan Bakari, Ahtari Humoud, Mohamed Isihaka, Abdallah Hassan, Hussein Mohamed, Juma Sadala, Said Kassim, Hamis Amour, Abubakar Abdallah, Salum Ali, Salum Amour, Alawi Othman, Rashid Ally, Amir Hamis, Kassim Salum na Said Shehe.
Kwa pamoja wanadaiwa kuwa kati ya Januari 2013 na Juni, mwaka huu walipanga njama ya kutenda makosa hayo na kuwezesha kufanyika kwa vitendo vya kigaidi.
Katika kipindi hicho na maeneo tofauti nchini, Sheikh Farid anadaiwa kuwa aliwaingiza Sadick Absaloum na Farah Omary nchini ili kushiriki kutenda makosa ya ugaidi.
Pia Sheikh Farid anadaiwa kuwa kwa makusudi na akijua kuwa anatenda kosa alitoa msaada kwa watu hao kutenda vitendo vya kigaidi kinyume cha sheria na anadaiwa kuwa katika kipindi hicho akiwa anajua kuwa Sadick na Farah wametenda makosa ya kigaidi, aliwahifadhi.
Mwananchi

5 comments:

Anonymous said...

Wazanzibari inabidi tuamke bila kujali itikadi za kisiasa. Leo ni viongozi wa Uamsho, kesho ni mimi na kesho kutwa ni wewe unayeshabikia matendo kama haya.

mungu awalani wote waliowatendea matendo haya masheikh wetu hapa hapa duniani na kesho akhera amin.

Anonymous said...

Hii ndio maana hao viongozi wa Uamsho wakapelekwa Tanganyika, kwa sababu wakoloni walihisi kuwa si rahisi kwa Mzanzibari mwislamu, kuweza kuwafanyia vitendo vya kinyama kama hivyo.

Mwamko pia unahitajika kwa wananchi. Tuangalie hivi karibuni nchini Marekani, katika jimbo La Missouri, askari polisi wakizingu alimpiga risasi na kumua kijana mweusi. Watu walitaka atajwe ni ni askari gani aliyefanya unyama ule, lakini wakuu waliendelea kulificha jina lake kwaisingizio cha usalama wake. Mji haukukalika, vijana waliingia mitaani. Polisi walishindwa kudhibiti hali ya mambo, jeshi likaletwa, vijana ngangari na madi yao, mpaka jina la askari likatolewa. Mpka sasa hivi hali bado ni tete.

Jee Wazanzibari tumeshafikia kiwango cha mwamko kama huo? Mara nyingi mitandaoni panapotolewa hoja ya watu kuingia mabarabarani, mimi huwa nauhafidhina kidogo. Kwa sababu wengine tunaandika tukiwa nje ya Zanzibar, watu yakiwakuta letu ni kulaani tu.

Bado nasisitiza mwamko wa umma na umoja unahitajika, palipofika panatosha!
Kwa upande mwengine, watu walisema, kadiri giza linapokuwa nene, alfajiri inakaribia. Na Adam Shafi katika kitabu chake cha Kuli alisema, “yana mwisho haya”. Lakini mwisho wake umomakilini mwetu!

Naomba kuwasilisha

Anonymous said...

Kwa vovote lazima action ifanyike sasa wakati wa kuwongeya sana umekwesha ni vitendo .Hatuna viongozi wa kweli kazi domo tu. Raiya wanachukuliwa ovyo wamekaa. Serekali imekaa . Hii yoyote inatokana mfumo mbovu unawoendeswha na hawa wanaojita waislam jina tu maCCM. Ni lazima achaguliwe mmoja kindakindaki atuwongoze na kazi Halafu tumlinde kisawasawa jeshi likija kutafuta tunaanza mkakati . Lazima hii najis CCm tuifute mara mmoja

Na nyinyi mnaojita baraza la wawakilishi basi mara hii mtalita baraza la mapishi au la matapishi kumbavu wamoja .

Anonymous said...

Dr.shein tangu siku aliyokaa madarakani watu wamekuwa wakisumbuliwa kwa kukamatwa ovyo-ovyo hasa Masheikh, Wapemba na wapinzani, kwa kuwekwa ndani kwa kesi za kubambikiziwa uongo.

Kiongozi wa nchi aliyekula kiapo cha kuitumikia Zanzibar na raia wote wa Zanzibar, hivi kweli ndiyo anawalinda na kuwatumikia. Dk Shein, bila kumchambua sana ana chuki ndani ya moyo wake dhidi ya Wazanzibari.

Inshaallah hawa wenye kufanyia masheikh wetu hivi, Mungu awajaaliye watembee na shuka maisha suruali wasiithubutu. kwa maana yakuwa wasimike tu yawe ndio maisha yao.

Tunahitaji tusome dua na kuka itkhaf na kuiombea nji yetu na masheikh wetu na Allah atatulipia.

leo wao kesho huenda ikawa sisi tusifanye mashkara na hatuna raisi sisi wakututetea zaidi ya Allah.

Anonymous said...

Too late, too late. Watu hawa wamo ndani karibu miezi miwili sasa na khabari za ukatili waliofanyiwa zimezagaa mitaani. Siku ya Iddi pale Lumumba ilitajwa hadharani kadhia yao. Ndo kwanza mnalalama leo. Taarifa yenu kwa vyovyote wataipuuza haina lolote la kuwatisha.

Tuanze kuzitia moto office za muungano zanzibar, na kuwanyemelea viongozi wa smz pamoja na huyo DPP, kwa hivi sasa maandamano ya nguvu yafanyike.

Mahakama za zanzibar Pia tuzitie moto kwa sababu hazina maana yoyote, Zaidi ya kuwanyanyasa wazanzibari.


Tunamuomba Allah awape ustahamilivu na nguvu masheikh wetu, na amlipe kila aliyeshiriki katika dhulma hii hapa hapa duniani na amzidishie adhabu kesho akhera. Amin.