Viongozi wapya wakiwa katika picha ya pamoja na Balozi Kilumanga. Mwenye kanzu kulia mwa Balozi, Bw. Salum Ali Abdallah (Mwenyekiti), wa kushoto kutoka alipo Balozi ni Bw. Khalfan Salum Khalfan (Makamu Mwenyekiti) anayefuatia kushoto ni Bibi Rukia Selemani (Katibu).
Jana tarehe 10 Agosti 2014, Watanzania wanaoishi katika Muungano wa Visiwa vya Comoro waliamzisha rasmi Jumuiya yao. Lengo la kuanzishwa kwa Jumuiya hiyo ni kuwaunganisha wanachama wake, kuwawezesha kushirikiana katika kutambua fursa za maendeleo na kutoa mchango kwa taifa lao la Tanzania.
Mkutano huo ulifanyika katika Ukumbi wa Mikuta wa Ubalozi wa Tanzania, Moroni.
Wakati akifungua mkutano huo, Mhe. Chabaka Kilumanga, Balozi wa Tanzania nchini Comoro aliwaeleza Watanzania hao kwamba Serikali ya Tanzania inathamini sana na kutambua mchango wa raia wanaioshi nje nchi.
Kutokana na kutambua umuhimu wao Serikali imeanzisha Idara inayoshughulikia Watanzania wanaoishi Ughaibuni katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Aidha, Kitengo kama hicho kimeanzishwa katika Ofisi ya Rais wa Zanzibar. Sambamba na hilo, Viongozi wote wamekuwa wakikutana na Watanzania wanaoishi Ughaibuni, kila wanapata fursa ya kufanya hivyo, wanapokuwa nje ya nchi.
Mkuu wa Utawala wa Ubalozi, Nd. Ali Jabir Mwadini alitoa mada kuhusu misingi ya uanzishaji wa Jumuiya za Kiraia na kubainisha vipengele muhimu vinavyopasa kuzingatiwa husasan katika katiba ya Jumuiya.
Mwisho, ulifanyika uchaguzi wa viongozi wa muda waliopewa jukuma la kuandaa katiba.
1 comment:
Kweli DMV mmeleta mwamko! Wanadiaspora WaTanzania tunanguvu kubwa saana ya kuchangia maendeleo nchini mwetu.
Post a Comment