Advertisements

Monday, September 1, 2014

Balozi Mdogo wa Tanzania- Dubai Mhe. Omar Mjenga akutana na kufanya mazungumzo na Mhe. Hamad Buamim, Rais na Mtendaji Mkuu wa Dubai Chamber of Commerce and Industry.

Katika mazungumzo, wamejadiliana uwezekano wa kuwa na ziara ya kibiashara kwenda Tanzania, kwa makampuni na viwanda vilivyopo Dubai, ili kukutana na wafanyabiashara na wamiliki wa viwanda Tanzania, ili kujionea na kuibua fursa za uwekezaji. Wamekubaliana ziara hiyo ifanyike mwanzoni mwa mwaka kesho na hivyo basi kuanza maandalizi mapema.

Mwezi Novemba, kutakuwa na ziara ya kibiashara ya makampuni kutoka Falme ya Ajman.

Aidha, wamezungumzia kuhusu mkutano wa Africa Global Business Forum utakaofanyika tarehe 1-2 Oktoba 2014 hapa Dubai. Mtukufu Sheikh Mohammed bin Rashid al Maktoum amemwalika Rais Kikwete kuhudhuria pamoja na marais wengine wa Mali, Ghana, Uganda, Mozambique, Ethiopia, Senegal, Burkina Faso, Sudan na Ivory Coast.

Mkutano huu hufanyika kila mwaka ambao huzungumzia njia muafaka ya ushirikiano kati ya Serikali ya Dubai na UAE kwa ujumla na nchi za Afrika.

2 comments:

Anonymous said...

Sasa Luka sasa unaabania comment za nini

Anonymous said...

is this self promotion? What is balozi mdogo, who is the actual balozi we never see or hear from him/her