ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, September 2, 2014

BONDIA FRANCIS MIYEYUSHO KUPAMBANA NA EMILIO NORFAT MKWAKWANI TANGA

Bondia Francis Miyeyusho kushoto akitunishiana misuli naEmilio Norfat baada ya kusaini mkataba wa kuzipiga Oktoba 5 katika uwanja wa Mkwakwani Tanga mpambano wa raundi nane katikati ni Mratibu wa mpambano huo Anton Rutta Bondia Francis Miyeyusho kushoto akitunishiana misuli naEmilio Norfat baada ya kusaini mkataba wa kuzipiga Oktoba 5 katika uwanja wa Mkwakwani Tanga mpambano wa raundi nane makubaliano hayo yalifanyika Dar es salaam jana 

Mabondia Emilio Norfat wa pili kushoto akitia saini ya kupambana na 
Francis Miyeyusho kulia katika mpambano utakaofanyika 
Oktoba 5 katika uwanja wa Mkwakwani Tanga mpambano wa raundi nane makubaliano hayo yalifanyika Dar es salaam jana wengine ni Ibrahimu Kamwe na Anton Rutta 

Na Mwandishi Wetu
BONDIA anaeshikilia nafasi ya pili kwa ubora nchini katika uzito wa featherweight kg 57 Emilio Norfat anaefanya shughuli za kupigana nnje ya nchi mara nyingi ameapa kustafisha ngumi bondia Fransic Miyeyusho watakapo zidunda siku ya
Oktoba 5 katika uwanja wa Mkwakwani Tanga mpambano wa raundi nane

bondia huyo mwenye rekodi ya kupambana mapambano 27 ambapo ameshinda 23 na kupoteza mapambano 4 ameapa kamwe ato kubali kupeteza nafasi hiyi adimu kupatikana ambayo alikuwa akitafuta siku zote akizungumza na waandisha wa habari mara baada ya kutia saini mkataba wa kuzxipiga na Miyeyusho alisema mimi ni namba mbili yeye ni namba moja kwa Tanzania hii hivyo nikimpiga tu mimi ndio nakuwa nashikilia usukani katika nchi hii

nae bondia Francis Miyeyusho anaeshikilia nafasi ya kwanza kwa ubora nchini amecheza mapambano 51 ameshinda 38 na kupoteza 11 na mapambano 2 akitoa droo

amesema ayupo tayali kabisa kupoteza mpambano huo utakaopigwa katika jiji la Tanga uwanja wa Mkwakwani na kuwataka mashabiki wake wote nchini kumuunga mkono kwa kwenda kuangalia ngumi siku hiyo ambayo ni mara yangu ya kwanza kucheza katika mkoa huu

siku hiyo pia kutakuwa na huuzwaji wa
DVD ambazo zinatoa mwanga kwa mchezaji kujua mchezo na kufahamu zaidi mbinu mpya zitumiwazo na mataifa mbali mbali Duniani.

Wakiwemo mabondia bingwa wa dunia kama Manny Paquaio,Floyd Maywether,Amir Khani, Mohamed Ali ,Mike Tayson na wengine wengi wanaotamba na waliotamba katika mchezo huo wa masumbwi Duniani

kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' ametoa wito kwa makampuni mbalimbali kujitokeza kutoa sapoti ya mchezo wa masumbwi kwani ndio mchezo pekee unaoweza kututoa kimasomaso watanzania tukafurahi

No comments: