Tuesday, September 16, 2014

Hitma ya Marehemu Jamila Abdallah Tumbo Maryland nchini Marekani

Kaka ya marehemu Ally Tumbo akijumuika na Watanzania wengine kwenye hitma ya mdogo wake Jamila Tumbo iliyofanyika Jumapili Sept 14, 2014 Silver Spring, Maryland nchini Marekani na kuhudhuriwa  na ndugu jamaa na marafiki.

Dr Seche (kushoto) akimfariji mmoja ya ndugu ya marehemu aliposhindwa kujizuia kwenye hitma ya ndugu yake Jamila Tmbo aliyefariki siku ya Jumapili Sept 7, 2014 katika hospitali ya Hindu Mandal jijini Dar es Salaam, Tanzania,

Msanii wa Bongo Movi, Aunty Ezekiel (kulia) akijumuika na Watanzania wa DMV kwenye kisomo cha hitma ya Jamila Tumbo iliyofanyika siku ya Jumapili Sept 14, 2014.

Mwanamuziki wa kizazi kipya Cassim Mganga akijumuika na Watanzania DMV kwenye hitma ya Jamila Tumbo.

Kaka ya marehemu Ally Tumbo akiwashukuru wana DMV kwa kujumuika na kuwafariji katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa mdogo wao.

Mudy Mabenzi (shati jekundu) akiendesha hitma huku akisaidiana na wenzake siku ya Jumapili Sept 14, 2014.
kwa picha zaidi bofya soma zaidi.

1 comment:

Anonymous said...

inna illahi waina illahim rajiun,poleni sana ndugu jamaa na marafiki wote wa wafiwa,kweli miyoyo mema ya kujumuika na wenzenu katika huzuni na starehee mungu akujaliyeni hivyo hivyo miyoyo yenye kheir na barka tele ya kushikana wana dmv wote.

jambo mmoja tu kama nasaha kwangu na kwenu pia hakuna aliye kamilika sote tuna mapungufu yetu so tujaribu kujirekebisha hasa hasa tunapokuwa katika majumuiko kama haya ya kumfariji mwenzetu mfiwa.

tunaposoma kitabu cha Allah tutulize macho yetu kwenye kitabu hicho tusiwe kuyatembeza kila pahali tunakosesha adabu hicho kitabu na tunatak rehma za Allah zitufikiye na sisi pia wasomaji so tuwe makini na kutuliza macho yetu kwenye kitabu hicho kitukufu.

na jambo la pili hata kama si dini yako basi jaribu kuvaa suruali usije na kikaptura si vizuri hata kama si dini yako ni mahali pa huzuni hapo na pia unavaa zizuri hivyo surali na kipuri/kihereni masikioni cha nini, basi kama ni pambo lako basi kivue ikimalizika hii shughuli ukitoka kivae..

tunakumbushana tu wote hatujakamilia na samahani kama nimewakosea wahusikia.

ahsante.

inna lillahi waina illahim rajiun. Allah akupeni moyo wa kustahamili wafiwa wote na wana dmv wote kwa msiba huu wa kipenzi ndugu yetu amuweka mahali pema peponi pamoja na kila muslimin wal muslimaat. Amin amin amin.