1.
UTANGULIZI
Binadamu
hakuumbwa katika ombwe, ameumbwa akiwa katika dimbwi la majukumu, kwake
binafsi, familia, jamii na dunia kwa ujumla. Wachache sana wanaoweza kupitia
ngazi zote za uwajibikaji huu. Katika hao wachache, hatutasita kumtaja Jakaya
Khalifan Mrisho Kikwete. Ili kujijenga vema katika misingi ya uongozi, Jakaya
Kikwete alijijenga vema katika taasisi hizi za msingi na alipikwa vema.
Mheshimiwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ni aina ya
kiongozi pekee ambaye alihudumu nafasi mbalimbali ndani ya chama na serikali.
Safari yake ya uongozi ilianzia ndani ya chama cha TANU. Alikuwa kiongozi wa
Vijana wakati wa TANU na baadaye CCM hadi kuwa Mwenyekiti wa Chama cha
Mapinduzi. Wakati wote katika nafasi
zake kwenye chama na serikali, Mh. Kikwete alihimiza maendeleo katika Jimbo
lake na watanzania kwa ujumla.
Kimsingi
amekuwa chachu ya maendeleo katika kipindi cha urais wake kuanzia mwaka 2005
hadi 2014 ambapo ameshatekeleza miradi mbalimbali ya kimaendeleo ambapo mingi
imeshakamilika na mingine inategemewa kukamilika mwishoni mwa mwaka 2015.
2.
HISTORIA
YA MAENDELEO
Kimaendeleo,
Tanzania ya mwaka 1961 si ya sasa. Tulipopata uhuru mwaka 1961, Tanzania ilikuwa
ni nchi changa ambayo haikuwa na mfumo thabiti wenye kuleta maendeleo. Hii ni
kutokana na athari tulizozipata wakati wa ukoloni mkongwe (Classical
Colonialism) na Ukoloni Mamboleo, Vita ya Kagera na Maanguko ya kimataifa ya Uchumi.
Hali hii iliathiri shughuli za maendeleo
kutokufanikiuwa kwa kiwango cha juu. Tanzania ilipitia kipindi kigumu kiuchumi
na vita mwaka 1977 mpaka 1979 ambapo ilipelekea athari zaidi kiuchumi hadi
miaka ya 1980 ambapo Tanzania ililazimika kukaribia soko huria ili kujenga
uchumi. Miaka ya 1990 mpaka miaka ya 2000 Tanzania imesonga mbele kiamendeleo
kutokana na juhudi mbali mbali marais ambao wamekuwa wakifanya katika vipindi
tofauti vya uongozi wao ambapo Nyerere kutoka 1962 mpaka 1985, Mwinyi kutoka 1985
mpaka 1995, Mkapa kutoka mwaka 1995 mpaka 2005 na kwa sasa tuna Mh. Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ambaye alianza
uongozi kama Rais kuanzia mwaka 2005 mpaka 2015.
3.
MAENDELEO
WAKATI WA AWAMU YA NNE CHINI YA UONGOZI WA JAKAYA KIKWETE
Akiwa na
dhamira ya kuhakikisha kwamba kila mtanzania anapata fursa sawa katika utumizi
wa rasilimali asili na watu zilizopo ili kumjengea uwezo kila mtanzania kufikia
kiwango cha maisha bora, Mh. Kikwete alinuia kuboresha maeneo ya msingi yatayowapeleka
watanzania katika kilele cha “MAISHA BORA”. Ili kuijenga barabara ya kuelekea
katika kilele hiki, awmu ya nne ya serikali yake ilitia mkazo katika maeneo
kadhaa kama ifuatavyo:
a)
Kukuza
utawala bora.
Mheshimiwa
Rais, ni dhahiri kuwa kiwango cha utawala bora katika nchi yetu kimezidi
kuimarika siku baada ya siku tena kwa ufanisi mkubwa tangu ulipoingia
madarakani. Hilo linathibitika zaidi kwa kuaangalia maeneo mawili makubwa
ambayo ni kupunguza urasimu katika shughuli mbalimbali za kiserikali ili
kurahishisha upatikanaji wa huduma kwa wananchi. Mashirika mbalimbali duniani
yamekuwa yakitambua mchango wako na kukuwezesha kutunukiwa nishani mbalimbali
ambazo hakika ulistahili, kama wasemavyo wahenga “ chanda chema huvikwa pete”
Kutokana
na uongozi wako mahiri, Tanzania imepata mafanikio katika nyanja za demokrasia
na utawala bora kama ambavyo Mpango wa Afrika wa Kujitathmini katika Utawala
Bora (APRM) umebainisha kwamba Tanzania ni kati ya nchi zinazofanya vizuri
kwenye eneo la utawala bora.
Tanzania imefikia katika kuridhia na
kutekeleza mchakato wa Kujitathmini katika Utawala bora kwa nchi za Afrika (APRM)
kuwa ni kuwashirikisha wananchi kutoa maoni yao kuhusu hali ya utawala bora
nchini na serikali kuruhusu wataalamu wa utawala bora kutoka nchi wanachama
kuja nchini kuhakiki mchakato huo.
Ni ukweli kuwa APRM ni mpango ulioasisiwa Machi 9,
mwaka 2013 na wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika (AU) ambapo Mheshimiwa
rais ulikuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha Tanzania inatoa fursa ya
kujipima na kujua mwenendo wa serikali na madereva wa utekelezaji (Viongozi wa
serikali)
Tanzania kwa sasa ni miongoni mwa nchi 34 kati ya
54 za AU zilizokwishajiunga na mpango huu, ikiwa imejiunga tangu mwaka mwaka
2004.
Suala la
elimu.
Elimu ni nyenzo ya msingi katika
jitihada za kujenga uchumi wa kisasa wa Taifa linalojitegemea na kuwawezesha
kiuchumi wananchi. Uchumi wa kisasa unahitaji watenda kazi wenye maarifa
yanayohusu kanuni na maarifa ya kumudu vitendea kazi vya aina mbalimbali.
Wanafunzi wanaojiunga na vyuo vikuu vilivyopo
nchini Tanzania waliongezeka kutoka 55,296 mwaka 2005/2006 hadi 118,000mwaka
2009/2010.Idadi ya vyuo vikuu imeongezeka kutoka vyuo vikuu 23 mwaka 2005 hadi
kufikia vyuo 31 mwaka 2010.
Kuweza kujenga chuo kikuu cha Dodoma chenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 40,000 kwa mwaka na kwa sasa kina wanafunzi 17,282
Wanafunzi wanaomaliza elimu ya msingi na kuendelea na elimu ya sekondari wameongezeka kutoka 493,636 hadi 999,070 huku idadi ya wanafunzi wanaogharamiwa na serikali toka familia zenye kipato duni ikiongezeka toka 16,345 hadi 58,843. Ongezeko hili ni kati ya mwaka 2005 hadi mwaka 2009. Pia Uandikishaji katika elimu ya awali umeongezeka kutoka wanafunzi 638,591 hadi wanafunzi 889,363.
Kuweza kujenga chuo kikuu cha Dodoma chenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 40,000 kwa mwaka na kwa sasa kina wanafunzi 17,282
Wanafunzi wanaomaliza elimu ya msingi na kuendelea na elimu ya sekondari wameongezeka kutoka 493,636 hadi 999,070 huku idadi ya wanafunzi wanaogharamiwa na serikali toka familia zenye kipato duni ikiongezeka toka 16,345 hadi 58,843. Ongezeko hili ni kati ya mwaka 2005 hadi mwaka 2009. Pia Uandikishaji katika elimu ya awali umeongezeka kutoka wanafunzi 638,591 hadi wanafunzi 889,363.
Tanzania imeweza kupiga hatua kubwa kwenye utaoji
elimu kwa wananchi wake. Kwa kupitia(Mpango Wa Maendeleo wa Elimu ya Msingi)
MMEM, MMES na MEMKWA; watoto wengi wa Kitanzania wamepata fursa ya kujiunga na
elimu ya msingi na sekondari. Hadi mwaka 2010 zaidi ya watoto milioni 8 (ambao
ni zaidi ya 90% ya uandikishaji halisi) wameandikishwa shule za msingi na zaidi
ya wanafunzi 1, 638, 699 wako sekondari.
Idadi ya shule na walimu imeongezeka maradufu. Hadi
mwaka 2010 shule za sekondari zimeongezeka kutoka shule 937 na kufikia idadi ya
4,2663 mwaka 2010. Walimu nao wameajiriwa kwa idadi kubwa ili kusaidia mchakato
wa kuwapatia watoto elimu. Kwa mfano, hadi mwaka 2010 idadi ya walimu wa shule
za msingi na sekondari imefikia walimu 206, 3734 kutoka idadi ya walimu 54,869
mwaka 2001. Ongezeko hili limechangiwa na ongezeko kubwa la wanafunzi kwa
kuanzia miaka ya 2001 hadi 2010.(tazama jedwali na 1). Hii ni dhahiri kuwa
fursa za elimu kwa wote zimeongezeka nchini, na hatuna budi kuipongeza serikali
chini ya Rais Jakaya Kikwete na wadau wa elimu kwa jitihada hizo.
Mafanikio katika sekta ya Afya
Mheshimiwa rais, tunapenda kukupongeza kwa kiasi
kikubwa kwa jitihada zako katika sekta hii muhimu katika taifa letu. Wote
tunafahamu maradhi ni moja kati ya maadui wakubwa ambao wanalisonga taifa letu
toka tupate uhuru.
Ni dhahiri kuwa tangu ulivyoingia madarakani
umekuwa ukipambana kwa dhati ili kuhakikisha mapambano juu ya maradhi
yanapungua kwa kiasi kikubwa. Wote ni mashahidi kwamba umepigania sana afya ya
mama na mtoto kwa lengo moja kuu ambalo lilikuwa ni kupunguza vifo vya kina
mama wajawazito pamoja na watoto kwani hicho kimekuwa ni kilio kikubwa na
tatizo kubwa ambalo linazikabili nchi zinazoendelea, kuna msemo usemao
ukimsaidia mwamke basi umeokoa jamii nzima, hivyo basi ni dhahiri kuwa kwa nia
yako hiyo umefanikiwa kuokoa jamii kubwa sana ya watanzaia wa kizazi kijacho.
Mheshimiwa Rais, umechangia kwa kiasi kikubwa
kupambana na ugonjwa wa Malaria ambao umekuwa tishio sio tu Tanzania bali hata
Afrika kwa ujumla lakini kwa jitihada zako za dhati kabisa toka moyoni ulikuwa
muhamasishaji namba moja katika kupiga vita ugonjwa huu. Ni ukweli usiopingika
kampeni mbalimbali kama vile “zinduka”
na zingine ambazo zilibeba dhana ya kuhamasisha jamii kutumia chandarua
zimekuwa na mchango mkubwa sana katika jamii yetu.
Mheshimiwa Rais, vilevile umetoa mchango mkubwa
sana katika vita dhidi ya ugonjwa hatari kabisa wa ukimwi kwani wakati unaingia
madarakani ugonjwa huu ulikuwa ni tishio sana lakini kwa jitihada zako
umefanikiwa kwa kiasi kikubwa kupunguza maambukizi kama ambavyo takwimu za tume
ya kudhibiti UKIMWI (TACAIDS) za mwaka 2014 zinatuonesha maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi nchini yamepungua
hadi kufikia asilimia 5.1 kwa mwaka 2011/2012 ambapo asilimia 6.2 ni
wanawake na asilimia 3.8 ni wanaume.
Mheshimiwa Rais, katika awamu zako
mpaka sasa umejitahidi kwa kiasi kikubwa Katika kuyaendeleza makundi
mbali mbali ya kijamii,kwa namna moja ama nyingine, na katika hilo kuna
mafanikio ya moja kwa moja ambayo yanonekana kama vile
Wanawake.
Hatua ya kurekebisha sheria
zinazowabagua na
kuwadhalilisha wanawake katika usawa na
maslahi yao imetekelezwa. Sheria ya makosa ya kujamiiana na sheria ya
kuwalinda, wajane, zimerekebishwa na Sera ya Hifadhi na Maendeleo ya Wanawake,
ziliboreshwa na kusimamiwa kwa kiwango stahiki kwa mfano uanzishwaji wa BENKI
YA WANAWAKE pamoja na utoaji wa mikopo mbalimbali mfano mkopo kwa watu wa chini
maarufu kama “MABILIONI YA JK”. Pamoja na miradi maalum wa kuinua kipato
cha wanawake ili kupunguza ajira mbaya kwa watoto umeanzishwa.
Pia idadi ya wanawake katika
nafasi mbalimbali za juu za uongozi
imeongezeka katika kipindi cha 2010-215 kwa mfano nafasi ya spika wa Bunge
ambayo kwa sasa anahodhi mwanamke mheshimiwa Anne Makinda.... takwimu
zinaonyesha katika kipindi cha uongozi wako nafasi za wanawake bungeni ni......
ambayo ni sawa na asilimia.... ukilinganisha na mwaka....pia hata katika bunge
la katiba linaloendelea idadi ya wanawake ni... ..
Walemavu
Ili kulinda na kusimamia haki, usawa na maendeleo
ya watu wenye ulemavu, Baraza la Taifa la Maendeleo ya Watu wenye Ulemavu,
limeanzishwa chini ya uongozi wa Afisi ya Waziri Kiongozi. Aidha, Sera ya
Walemavu imepitishwa na rasimu ya awali ya Sheria ya Walemavu imekamilika.
Hatua za kuelimisha jamii juu ya masuala mbali
mbali ya kuwaendeleza watu wenye ulemavu, zimetekelezwa. Jumla ya watu 219
wenye ulemavu wamepatiwa mafunzo ya uendeshaji wa biashara ndogo ndogo Unguja
na Pemba pamoja na kupatiwa mkopo wa kujiendeleza. Watu 193 wenye ulemavu wa
kutosikia (viziwi)
wamepatiwa mafunzo ya lugha ya ishara.
Miundo mbinu
Kipindi cha miaka kumi iliyopita cha 2000 – 2010 tumeshuhudia
kuwepo kwa
ujenzi mkubwa wa miundombinu ya barabara, viwanja
vya ndege na madaraja nchini. Miradi yote ya ujenzi ambayo haikukamilishwa kati
ya 2000 – 2005 imekamilishwa kati ya 2005 – 2010 na kuanzishwa ujenzi wa miradi
mipya kitakwimu, ujenzi wa miradi 15 kwa kiwango cha lami yenye jumla ya urefu
wa Km. 1,398.6 imekamilishwa katika kipindi cha 2005 - 2010. Aidha, ujenzi
ambao unaendelea ni wa miradi 29 ya barabara zenye jumla ya Km. 2,536.4 na
wakati huo huo miradi 7 ya barabara yenye jumla ya Km. 1,562 inaendelea
kufanyiwa upembuzi yakinifu kwa ajili ya ujenzi. Hiki ni kielelezo dhahiri cha
mafanikio makubwa ambayo yameiweka nchi yetu katika chati ya kuwa na miundombinu
ya kisasa ya barabara. Mwelekeo wa Sera
za serikali yako katika miaka ya 2010 hadi 2020 umeainisha jukumu
kubwa la nchi yetu katika kipindi hiki ni kutekeleza lengo la Dira 2025 la
kuleta mapinduzi ya uchumi yatakayoitoa nchi kutoka kwenye dimbwi la uchumi
ulio nyuma na tegemezi na kuiingiza katika mkondo wa uchumi wa kisasa wa taifa
linalojitegemea.
Dhana ya Kujenga Uchumi wa Kisasa inalenga katika
modenaizesheni ya uchumi.
Modenaizesheni kimsingi ni kuongeza maarifa na
matumizi ya sayansi na teknolojia
katika sekta za uzalishaji. Modenaizesheni ya
uchumi inalenga katika kuongeza
uzalishaji, ufanisi na tija katika uchumi hususan
katika kilimo, ufugaji, uvuvi na
viwanda.
Mapinduzi ya Kilimo
Kilimo ndio msingi wa uchumi wa kisasa na njia
sahihi ya kuutokomeza
umasikini.
Mheshimiwa rais umekuwa muumini wa dhati kwamba
kilimo cha kisasa
kinachotumia Kanuni na zana bora za kilimo ndio
ufunguo wa maendeleo ya
uchumi wa nchi yetu. Kilimo cha kisasa kina uwezo
wa kutoa mazao mengi zaidi
kutoka kila ekari iliyolimwa. Kwa nchi yetu, ziada
hiyo ya mazao ina faida kubwa
zifuatazo:-
(a) Kuipatia kila familia, kijiji na Taifa chakula
cha kutosha ili kukomesha njaa.
(b) Kulipatia Taifa mavuno mengi ya kuuza ili
kupata fedha za kigeni kwa ajili
ya maendeleo ya nchi.
(c) Ziada ya mazao huunda mazingira muafaka ya
kuanzishwa viwanda vya
usindikaji na utengenezaji wa bidhaa za viwandani.
(d) Familia yenye ziada ya mazao huutokomeza
umaskini kwa kuuza ziada
hiyo kwenye soko na kupata fedha za kujiletea
maendeleo.
32. Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita ya
utekelezaji wa Ilani ya mwaka 2005-
2010, Serikali zetu zilichukua hatua kubwa katika
kukipatia kilimo mwelekeo wa
kisasa ili kiondokane na zana duni, mashamba
madogo, kutozingatia kanuni bora
za kilimo na kuridhika na mavuno ya kujikimu.
Mheshimiwa Rais, kwa heshima na taadhima tunapenda kukupongeza kwa dhati kwa kuanzisha
mchakato wa Katiba mpya licha ya changamoto zilizojitokeza katika mchakato huo.
Sote tunatambua nia yako ya dhati kuhakikisha taifa letu linapata katiba mpya
kabla hujamaliza awamu yako ya pili ya uongozi hapo mwakani. Tunakusihi
mchakato huu usiwe chanzo cha machafuko nchini mwetu bali maridhiano ya kisiasa
yawe ndio msingi mkuu wa kupatikana kwa katiba itakayolivusha taifa letu kwa
miaka mingi ijayo. Mwisho tunakutakia safari njema na mafanikio tele katika
kutekeleza majukumu yako.
4.
CHANGAMOTO
a)
Kushuka kwa thamani ya shilingi
Shilingi
ya Tanzania imekuwa haijatengamaa kwa vipindi tofauti tofauti ukilinganisha na
Dola ya Kimarekani. Hali hii haijawa chachu katika juhudi za kimaendeleo
zinazofanyika. Katika suala la kushuka kwa thamani ya shilingi, Serikali
inatakiwa kujenga uchumi imara uliojengeka kwenye shilingi iliyoimara
ukilinganisha na Dola ya Kimarekani
b)
Bajeti isiyotosheleza mahitaji
Bajeti ya
Tanzania imekua isiyojitosheleza hasa kwa kuwa ni bajeti tegemezi. hii imesasababisha mambo mengi
kukwama. wahisani wengi wamekua hawaleti
pesa kwa wakati au kuleta fedha kwa masharti magumu yanaitesa nchi. Vyanzo
vingi vya mapato vimekua visivyotosheleza na hivyo kupelekea bajeti ya
maendeleo kuwa finyu ukilinganisha na mahitaji. Katika suala hili tunaishauri, Serikali ibuni vyanzo vipya na
vya mbadala vya mapato ili kukusanya fedha ya kutosha itakayotoshereza mahitaji
ya kibajeti
c)
Rushwa na ufisadi,
hili ni
tatizo na tishio katika maedeleo ya Tanzania, viongozi wengi katika sekta
mbalimbali Serikalini na hata sekta binafsi wamekuwa si waaminifu tena.
Wamekuwa wakidai rushwa za aina tofauti au kufanya ufisadi, ubadhirfu wa fedha
na hivyo kuathiri kwa kiasi kikubwa kasi ya maendeleo katika sekta mbalimbali.
d)
Kushuka kwa uzalendo
Watanzania
wa sasa si wa zamani. Zamani kulikuwa na misingi ya kimaadili na mafunzo
iliyopelekea watanzania wengi kuipenda nchi yao na hivyo kupelekea kuwa
wazalendo. Hali si hivyo tena kwa sasa, hii ni kutokana na kuibuka kwa
changamoto mbalimbali za sayansi na teknolojia hivyo kumepelekea watu kuwa
wabinafsi zaidi kuliko kujali masuala yanayohusu watanzania kwa jumla.
5.
HITIMISHO
Mwisho
kabisa mheshimiwa Rais, tunapenda kutoa pongezi zetu za dhati kwa kutunukiwa
nishani mbalimbali kutoka sehemu tofauti duniani ikiwa ni ishara ya wao
kutambua mchango wake baadhi ya nishani hizo ni kama Nishani Ubora wa Lulu ya
Afrika (Bwana tukufu) Julai 2007 Nishani ya Hilali Kijani ya Komori Machi
2009,Nishani ya Abdulaziz Al Saud ,Aprili 2009,Nishani ya Ubora Novemba
2009 ,Nishani ya Oman , Oktoba 2012 pamoja na tuzo za hivi karibuni
za Tuzo la Nyota wa Demokrasia Afrika 2014 – Icon of Democracy Award
Winner for 2014 in Africa
Wewe
ni kioo kwetu kama vijana na wapiganaji wengine wote, tutakufanya mwenye
tabasamu siku zote kwa kuishi uvumilivu wako wa kisiasa na kiumbe kinachopenda
mwafaka pale maslahiya kitaifa yanapotamalaki.
Wenu Mtiifu,
Loveness
Mamuya – Kada Mzalendo CCM Marekani