Advertisements

Monday, September 15, 2014

KINANA ASHIRIKI SHUGHULI ZA KIJAMII KIBITI


 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimtwisha maji mkazi wa kijiji cha Muyuyu Bi.Zainabu Athumani mara baada ya kuzindua mradi mkubwa wa maji utakaonufaisha wananchi 3765.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki zoezi la kuchanganya dawa kwa ajili ya kutengeneza batiki kwenye kikundi cha akina mama kinachoitwa Upendo.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia kitenge cha batiki alichotengeneza kwa kushirikiana na akina mama wa kikundi cha Upendo kitongoji cha Songa kijiji cha Mchukwi.
 Katibu Mkuu wa CCM akishiriki kupiga marimba na  wasanii wa kijiji Mchukwi wakitumbuiza ngoma ya Dega
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozana na mmoja wa mama lishe wa soko la Kibiti mjini ambapo alijionea namna ambavyo biashara zinavyoendelea.

No comments: