ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, September 9, 2014

KUNA AFADHALI UKIMFUMANIA MUMEO NA DEMU MZURI KULIKO ANAYEPAKA WANJA WA 'SINA BWANA' -2

MPENDWA msomaji, wiki iliyopita katika mada yetu ya Kuna afadhali ya kumfumania mumeo na demu mzuri kuliko anayepaka wanja wa ‘sina bwana?’ tuliishia kwa simulizi ya dada Mwanaidi Mkwazu, mkazi wa jijini Dar ambaye alisema kwa upande wake iliwahi kumtokea alimfumania mume wake akiwa na demu bomba.


TUJIKUMBUSHE
“Nilipenda awe amenizidi maana kama nitakuwa nimemzidi nitamshangaa sana mume wangu. Kufika kweli alikuwa msichana mzuri sana, simwingii kwa hata chembe. Kidogo hiyo ilinishusha hasira na wivu,” anasimulia Mwanaidi Mkwazu, mkazi wa Sinza, Dar.
Tunaendelea…

NI KWELI?
Kinachoonekana hapo ni nini? Ni udhaifu wa fikra. Siamini kama kweli haiba ya mtu inasaidia kwenye fumanizi. Kwamba eti ni afadhali umfumanie mwenza wako akiwa na ‘mwizi’ wa maana kuliko kumkuta na mwizi ‘oheahe’!!

Dhana hii naifananisha na watu wawili waliopata ajali kwa nyakati tofauti ya kugongwa na magari na kulazwa kwenye wadi moja halafu mmoja anamuuliza mwenzake ‘wewe umegongwa na gari gani?’ mwenzake anamjibu, ‘Toyota Vitz’, yule mwingine acheke na kusema, ‘kumbe afadhali mimi nimegongwa na Mercedes Benz.’ Kugongwa ni kugongwa tu hata kama itakuwa Bajaj ni kugongwa.

USALITI MBAYA
Umfumanie mumeo na hausigeli, umfumanie na malaya wa mtaani, iwe mfanyakazi wa benki maarufu au hata na daktari wa hospitali kubwa ni kitu kimoja tu kwani kilichofanyika hapo ni usaliti, afadhali inatoka wapi? Kuingiza afadhali ya haiba kwenye fumanizi ni kupungukiwa na uwezo wa kujitambua.

ITAKUSAIDIA
Naamini kwamba, kumfumania mume wako na mwanamke ‘mchovu wa sura na mwonekano au hao wa kupaka wanja wa ‘sina bwana’ inaweza kukusaidia wewe mwanamke kupitia upya nyendo zako katika ndoa au uhusiano.

Kivipi? Kwamba, inawezekana mumeo hana tabia ya usaliti lakini analazimika kufanya hivyo kwa sababu unamtilia ‘ngumu’ kitandani, sasa aende wapi! Matokeo yake anajitwalia mzoga wowote ule.

Ni kama vile mtoto aliyenyimwa chakula nyumbani kwao, akatoka nje akiwa na njaa, ni rahisi kujikuta akila kwa jirani chakula ambacho kwake au katika familia aliyotoka ni haramu.

Upo ushahidi wa kutosha kwamba, mwanamke anapomfumania mume wake akiwa na demu bomba hupata tabu kujua mumewe anapenda nini hasa! Kama anapenda uzuri, basi kuna dalili ya mume kuwa msaliti kila siku kwa vile siku hizi, wazuri ni wengi na wanaume wa kundi hili wagumu sana kuwadhibiti kuliko wale wanaojizolea chochote kwa sababu ya kutiliwa ngumu nyumbani kwani mke akijtambua usaliti hautatokea tena.

PAMOJA NA YOTE
Kwa leo naishia hapa lakini mada ya leo ilijaa ubinadamu wetu tu kwani katika usahihi usaliti hautakiwi kwa namna yoyote ile na ni vizuri wakati wote ndani ya ndoa au uhusiano kila mmoja akachunga nafasi yake ili kutotoa nafasi ya mwenzake kukengeuka!
GPL

No comments: