ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, September 9, 2014

KWA MADRIVER KAMA HAWA KILA SIKU WATAENDELEA KUTUMALIZA SERIKALI RUDISHA SHERIA YA KILA BASI LIWE LINASAFIRI NA TRAFFIC MMOJA AU POLISI.

Tabia ya kutojari sheria ndio sababu kubwa tunapoteza Ndugu wengi, Tunabidi kuilazisha serikali kuweka Divider katikati ya Barabara, kitu kibaya kinaweza kutokea hiwapo magari ya mwelekeo wa pili yakitokea.

2 comments:

Anonymous said...

Sidhani kama ni feasible kuweka traffic police kwenye kila basi kutokana na idadi ya mabasi kuwa ni kubwa na zaidi polisi wenyewe ni wala rushwa wakubwa.
Hii ni baadhii ya athari ya kuwa na utawala usiozingatia sheria,Kufumbia macho rushwa nazaidi ukosefu wa ethics kwa viongozi kwani walio wengi wana interest kwenye baadhi ya mabasi hayo.Hivyo tatizo ni kubwa zaidi ya tunavyo waona ma driver wanaover take, nila kimfumo zaidi.

Anonymous said...

Asante kwa kutupa.mwanya wa kutoa madukuduku. Kuna ishu kibao na hiyo picha. Tuchangie mawazo ya kulitatua hili na matatizo mengineo ya usalaama.
Kwenye hiyo njia hii option ya kuovatake ifutwe mara moja! Hela inayohitajika hapa ni us rangi na mpiga rangi.....kufanya hivi kutaokoa Maisha.
Kingepaswa kuwa kituo cha traffic kwa maana pana kona na mlima na lazima tu kutatokea na madreva wenye haraka na wasiojali maisha ya watu. Tunahitaje leseni zao zichukuliwe, tutangaziwe na picha zao ziwekwe mtandaoni iliwasipate kazi nchini.
ikiwawatapewa kazi lazima tumbane tajiri wake, huyo dreva na trafiki wa huo mkoa au mji mhalifu atakokamatwa safiri ya pili.
Wasafiri amkeni, saidia na wewe usaidiwe. Pigeni picha za madereva kama hawa ili msafiri mwenzako awe na uamuzi wakuokoa maisha yake.
Trafiki fanyeni kazi zenu, mnazikumbuka ? Lazima ujue sheria na adhabu yake. Fanyeni hivyo na swala la omba omba litakwisha yaani hongo.
Hongo ndiyo imezalisha balaa za barabarani, na nyie matrafiki mume halilisha haya madhambi mumemea huu utovu wa nidhamu.
Mishara midogo eh ? Lazima itakuwa midogo kwa maana nye hamjaliani. Hivi mnajua faini zinasaidia mfuko wa kitengo cha usalaama ikiwemo bajeti ya mishara yenu ?
Amkeni fanyeni kazi yenu na mtaona mishahara inapanda.
Trafiki fanyeni kazi yenu, acheni kuaibishana na kutuaibisha, Africa mashariki mnaongoza kwa utovu wa nidhamu.
Madereva okoeni maisha, si sifa kukimbiza gari ilimradi una ovateki.
wasafiri PIGENI UKUNGA, MAYOEE, SIMU NA PICHA na mkifika kituo cha polisi piga ripoti, chukueni lesseni number bima n.k ya hilo gari. Pigeni picha. Jioni au ukiwa na mtandao tumeni ripoti kwenye Blogu. Wote tukiwa wakali hili halitakuwa tatizo.
O na mkiwa barabarani trafiki akiwapiga faini tumeni ujumbe maana matatizo mengine kama matairi mabovu ni vizuri watu wajue wakwepe kupanda hayo mabasi.
Tushurikiane, kila kundi likiisukua lingine kwa mfumo wa checks and balances kila mtu ataokoa maisha ya watu, hongo itakuwa na madhara ama adhabu, wamiliki watakuwa makini zaidi, madereva wengi watafikiria mara mbili mbili kabla ya kufanya kosa.
Tuanze kuyatekeleza leo.