Advertisements

Thursday, September 18, 2014

MAOFISA WA TBL WAKAGUA MIRADI YA MAENDELEO INAYOWEZESHWA NA ACE AFRICA CHINI YA UFADHILI WAO

Mwenyekiti wa Kikundi cha Tumaini Saccos, akiwaonyesha namna sanduku maalumu lakutunzia taarifa za kikundi chao linavyolindwa, wakati maofisa wa Kampuni ya Bia Tanzania walipokwenda hivi karibuni kukagua miradi mbalimbali ya wananchi wilayani Arumeru inayowezeshwa na Taasisi ya ACE AFRIKA kwa ufadhili wa TBL.
Mwanachama wa Tumaini Saccos ambaye pia ndiye Mwenyekiti wa kikundi hicho akionesha baadhi ya shughuli anazozifanya ambazo amewezeshwa na ACE AFRICA  chini ya ufadhili wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL). Maofisa wa TBL walikwenda hivi karibuni kukagua miradi ya kikundi hicho.
Mkulima wa bustani ya ndizi na mboga za majani, Isaya Supuk wa kijiji cha Olmotonyi, wilayani Arumeru, Arusha akiwaonyesha maofisa wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) na ACE AFRICA namna shamba lake lilivyostawi wakati maofisa hao wa TBL walipokwenda hivi karibuni kukagua shughuli hizo zilizofadhiliwa na kampuni hiyo.
Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),  Editha Mushi akizungumza na Mkurugenzi wa ACE AFRICA (TANZANIA), Joanna Waddington ofisini kwake Arusha, hivi karibuni kuhusu ufadhili wao unaowezeshwa na taasisi hiyo kwa wananchi wa Arumeru katika shuguli mbalimbali za maendeleo.

No comments: