ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, September 25, 2014

MAONI YA MWIGULU NCHEMBA,FEDHA ZOTE ZILIZOSALIA BUNGE LA KATIBA ZIELEKEZWE KWA WALIOKOSA MIKOPO ELIMU YA JUU

EXCLUSEIVEEEEE KUTOKA DODOMA
COMRADE MWIGULU NCHEMBA AKATAA FEDHA ZA UMMA ZILIZOBAKIA BUNGE LA KATIBA KUTAFUNWA NA WAJUMBE WA BUNGE HILO,AAGIZA FEDHA ZOTE ZILIZOSALIA BUNGE LA KATIBA ZIELEKEZWE KUSAIDIA WANAFUNZI WALIOKOSA MIKOPO ELIMU YA JUU,KUJENGEA VITUO VYA AFYA NA KUSAIDIA MASIKINI.
Mwigulu Nchemba asema fedha zitakazookolewa kutokana na kutokuendelea bunge maalumu zipeslekwe kuwalipia ada vijana waliokosa mikopo ya elimu ya juu.

Sokoine wa Pili ndugu Mwigulu Nchemba ameshauri fedha zitakazookolewa/kubaki baada ya kutokuendelea kwa mchakato wa katiba zipelekwe kuwalipia wanafunzi waliokosa mikopo ya elimu ya juu. Alipopigiwa simu na kama ilivyoripotiwa na magazeti Mwigulu amesema Mwaka jana wanafunzi zaidi ya 12,000 watoto wa masikini walikosa mikopo. Na kwa mujibu wa bodi ya mikopo mwaka huu huenda wanafunzi zaidi ya 28,000 watoto wa masikini watakosa mikopo ya elimu ya juu na kukosa fursa ya kwenda vyuoni. Mwigulu a.k.a (SOKOINE WA II) ambaye amejipambanua mioyoni mwa watanzania kuwa ni MTETEZI WA WANYONGE asiyeyumba wala kuogopa inapofika jambo la kuwatetea wanyonge, kusimamia fedha za kidi za wanyonge na kuhskikisha keki ya Taifa inagawanywa usawa na kuwafaidisha watanzania wote hasa masikini ili waweze kutoka kwenye dimbwi la umasikini amesema ni vyema watoto wa masikini hawa wapewe mikopo. " Kuna watoto karibu elfu 40 ukijumlisha na wa mwaka jana watakuwa wamekosa mikopo, mimi niliyetokana na familia masikini ningekosa mkopo ndio ungekuwa mwisho wa maisha yangu ya shule, ndoto ya chuo kikuu ingeishia hapo, na leo nisingekuwa hapa, TUKUMBUKE FAMILIA ZA AINA HIYO BADO ZIPO NA KATI YA WATOTO WALIOKOSA MIKOPO, WALE WANAOFANANANA NA ILOYOKUWA HALI YANGU WAPO," kwa kumbukumbu hiyo najiweka nafasi yao, nashauri fedha hizo zibadilishiwe matumizi zipelekwe bodi ya mikopo ili watoto wa masikini wapate mikopo. KUNA VIJANA WAMESOMA SHULE ZA KATA WAMELIPIWA ADA NA WAJANE WANAUZA VITUMBUA NA MATEMBELE WAKAFAULU NA KIDATO CHA TANO NA SITA WAKASOMESHWA NA WAJANE WAKAFAULU NA KUDAHILIWA VYUO VIKUU, ONLY WANAJIKUTA NDOTO YA KUFIKA CHUO KIKUU INAYEYUKA KWA KUKOSA MIKOPO.

Mwigulu akichangia bungeni alikataa waziwazi bungeni kuwa bunge lisiongezewe siku 24, licha ushauri huo kukataliwa aliposhauri lakini baadae mhe Rais aliagiza bunge liishie tar 4 oct na zile siku 24 alizokataa Mwigulu zikafutwa. Jambo hilo limeokoa zaidi ya bilion 20, pia Mwigulu alishauri kuwa kama hakuna Maridhiano na kama hakuna akidi ya kupitisha rasimu iende kwa wananchi ni vyema bunge mchakato usitishwe na fedha hizo zikasomeshee watoto wa masikini. Kutokuendelea kwa mchakato wa katiba hatua ya kura ya maoni utaokoa karibu bilioni 75, nadhani kiobgozi huyu mwenye jicho la huruma na moyo wa huruma kwa masikini kutokana na kuujua umasikini kutokana na kuzaliwa na kukulia maisha ya kimasikini anaongelea bilion hizi ambazo ni karibu bilioni 100.

Juzi mwenyekiti wa bunge alitangaza kuwa watazitafutia matumizi pesa zote walizopangiwa kwenye bajeti kwa ajili ya mchakato wa katiba hadi ya hatua ya kura ya maoni.

Zipo tetesi bunge maalumu wamemwandikia barua Rais akubali wajumbe wagawane milioni ishirini (20,000,000) kila moja pesa zilizookolewa kutokana na mchakato kuisha. Mwigulu amekuwa akiamini kuwa njia nzuri ya kuwainua nasikini ni kuwasomeshea watoto wao.
Hivyo amekuwa akisema unatoza kodi kwa matajiri unasomesha watoto wa masikini, unatoza kodi kwa matajiri zitoe huduma kwa masikini sio kugawanwa na wenye uchu wa kujilimbikizia fedha.
Awali Mwigulu aliwahi kuwambia bungeni bila uoga mbunge anaeona laki tatu haitosha afungashe virago aende zake pale baadhi ya wabunge walipokuwa wakidai laki 3 kwa siku haitoshi hivyo walipwe laki 8 kws siku kwa siku 150. Mwigulu tunakuomvea, Mungu akuinue hata uwe Rais kwani moyo wako unahuruma na masikini.

Chanzo.Mahojiano na Uhuru Media.

1 comment:

Anonymous said...

Mungu akubariki, akupe maisha marefu babe, ili uokoe wengi. Amina