ANGALIA LIVE NEWS

Friday, September 12, 2014

PPF YAPONGEZWA KWA KUENDESHA MAMBO KISASA

Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari baada ya kutokea mkanganyiko wa kauli ya mmoja wa wajumbe wanaoshiriki kwenye mkutano wa 24 wa wanachama na wadau wa PPF, kuwa kampuni ya AtoZ haiwasilishi michango ya wanachama. Hata hivyo Erio alijibu hoja hiyo kuwa habari hizo sio za kweli na kwamba AtoZ wanawasilisha michango kwa wakati na kwamba hawana tatizo nao
Mjumbe kjutoka chama cha viziwi Tanzania, Daudi Kulagwa, akizungumza kwenye mkutano huo
Mkurugenzi Mkuu mstaafu wa PPF, Naftali Msemwa, ambaye alikuwa akisimami kikao cha asubuhi cha mkutano wa 24 wa wanachama na wadau wa PPF ulioingia siku ya pili kwenye ukumbi wa mikutano wa AICC jijini Arusha, Alhamisi Sept. 11, 2014
Mjumbe wa bodi ya wadhamini ya PPF, Mzee Baraza akipitia ripoti ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Mfuko huo kwenye mkutano wa PPF
Mkurugenzi wa Fedha wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Martin Mmari, akitoa mada kuhusu huduma za kifedha za Mfuko huo, wakati wa mkutano wa 24 wa wanachama na wadau wa Mfuko huo kwenye kituo cha mikutano cha kimataifa cha Arusha, AICC jijini Arusha, Alhamisi Septemba 11, 2014. Mkutano huo umeingia siku ya pili.
Mkurugenzin wa Operesheni wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Asumpta Malya, akitoa mada kuhusu huduma mbalimbali zitolewazo na Mfuko huo
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Posta, (TPB), Sabasaba Moshingi, akielezea fursa mbalimbali za kifedha zitolewazo na benki yake, wakati wa mkutano huo
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio, akifafanua baadhi ya hoja zilizotolewa na wajumbe wa mkutano
Wajumjbe wakifuatilia mkutano
Wajumbe wa bodi ya wadhamini ya Mfuko wa Pensheni wa PPF, Amelye Nyembe (Kushoto) na Mwamini Tully, wakionyeshana kitu kwenye jarida la ripoti ya mwaka ya Mfuko huo
Wakurugenzi wastaafu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Naftali Msemwa, (Kulia) na David Mataka, wakiwa kwenye mkutano huo
Mjumbe akisaidia kumpatia begi lenye nyaraka muhimu zinazohusu mkutano huo
Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudencia Kabaka, akizungumza kwenye mkutano huo
Mfanyakazi wa PPF, Herieth Magala, akigawa mabegi yenye nyaraka mbalimbali za mkutano wa 24 wa Mfuko huo
Mwenyekiti wa Mamlaka ya Udhibiti Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, SSRA, Ally Juma Muhimbi, akiwa mkutanoni
Wajumbe wakipitia taarifa mbalimbali za Mfuko wa Pensheni wa PPF, kwenye ukumbi wa Simba wa kituo cha mikutano cha kimataifa cha Arusha AICC

No comments: