Advertisements

Wednesday, September 24, 2014

RASIMU YA KATIBA ILIYOPENDEKEZWA NA BUNGE MAALUM 2014

Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samuel Sitta

Mambo yameiva, na hii hapa ndiyo Rasimu ya Tatu ya Katiba, ambayo inapendekezwa na Bunge Maalum. 
Vipengele vingi vimebadilishwa. Haya hapa ni mambo ya Muungano:
Mambo ya Muungano
1. Katiba na Mamlaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
2. Ulinzi na usalama wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
3. Usalama na usafiri wa anga.
4. Uraia na uhamiaji.
5. Jeshi la Polisi.
6. Sarafu na Benki Kuu.
7. Kodi ya Mapato inayolipwa na watu binafsi na Mashirika, ushuru wa forodha na ushuru wa bidhaa zinazotengenezwa nchini Tanzania na zinazosimamiwa na Idara ya Forodha.
8. Mambo ya nje.
9. Usajili wa vyama vya siasa.
10. Mahakama ya Juu na Mahakama ya Rufani.
11. Elimu ya Juu.
12. Baraza la Taifa la Mitihani na mambo yote yanayohusika na kazi za Baraza hilo.
13. Utabiri wa hali ya hewa.

14. Utumishi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano. 

IPAKUE MWENYEWE HAPA: RASIMU YA TATU

3 comments:

Anonymous said...

Mamlaka ya Serikali ya Jamhuri
ya Muungano
72. Serikali ya Jamhuri ya muungano itakuwa na mamlaka ya utekelezaji katika Jamhuri ya Muungano kwa Mambo ya Muungano na kwa mambo yote yasiyo ya Muungano yanayohusu Tanzania Bara. Mamlaka ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa mambo yasiyo ya
Muungano
73.-(1) Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itakuwa na mamlaka na haki juu ya mambo yasiyo ya Muungano yanayohusu Zanzibar.

Anonymous said...

URAIA PACHA

Hadhi maalum ya watu wenye asili
au nasaba ya Tanzania

69. Bila kuathiri masharti yaliyomo kwenye Sura hii, mtu yeyote
mwenye asili au nasaba ya Tanzania na ambaye ameacha kuwa raia wa Jamhuri ya Muungano kwa kupata uraia wa nchi nyingine, atakapokuwa katika Jamhuri
ya Muungano, atakuwa na hadhi maalum kama itakavyoainishwa katika sheria za nchi.

Kama ilivyo andikwa hapo juu,"..atakapokuwa katika Jamhuri
ya Muungano, atakuwa na hadhi maalum kama itakavyoainishwa katika sheria za nchi..." naona ni mafanikio makubwa sana kwa watu wanoishi ugaibuni kwa sababu wako huku kwa makundi mbalimbali na sababu tofauti. Ni matumaini yetu kwamba Serikali itatunga sheria ambazo hazina ubaguzi na zitazingatia usalama wa taifa kwanza,maendeleo ya kichumi na ujamii wa watanzania wote

Anonymous said...

hivi ni kwanini hili koti halivuliwi? wewe huyohuyo muungano nahapohapo wewe ni bara. maanayake Tanganyika tumekubali vipi kuivunja? kwani muungano uliopo ni watanganyika na Zanzibar na sio bara na Zanzibar. kwamaana hiyo muungano uitwe bara na visiwani kwasababu bara sio nchi. kwakweli haki haikutendeka kwani hakuna wakuulizwa mambo Tanganyika.