Sensei Magoma
Sensei Magoma ni mmoja kati ya wanafunzi wa tano nchini kupata shahada ya kwanza “Shodan” mkanda mweusi mwaka 1976 akiwa mwenye umri mdogo kulikoni wenzake wote chini ya sensei Bomani. Wanafunzi hao ni: Sensei Mapfumo Gamanya ( Mzibabwe), sensei Tola Sodoinde Malunga, Sensei Abome Mabruki na kaka yake sensei Adombe Mabruki, na mwisho kwa umri kati ya hao ni Sensei Magoma Nyamuko Sarya.
Wakati sensei Bomani akiwa nje ya nchi huko nchini Marekani kuanzia mwaka 1976 hadi mwaka 1981 sensei Magoma ndiye alikuwa mwanafunzi mkuu kiongozi na mwenye mamlaka yote ya mapendekezo na kutoa test na hata mikanda yote ya mtindo wa Okinawa Goju Ryu Kyokai chini ya mfumo wa kiongozi wao wa Karate duniani Master Eiichi Miyazato, mwalimu wa sensei Bomani. Vigumu mno kuwataja wanafunzo wote waliopitia chini yake, bali tu, kila mwanafunzi aliyekuwa dojo kwa miaka ya 1976 hadi 1982 alikuwa chini ya himaya yake.
Licha ya kuwa mkufunzi mkuu wa Karate nchini Tanzania, mara tu baada yakuondoka mwaka 1982 kwake hapa nchini kuelekea nchi za mashariki ya mbali ikiwemo, India, Nepal, Singapore, Malaysia,na Phillipines. Mwalimu Magoma alizcha pengo kubwa ambalo hadi hii leo hamna hatamwenye kuweza liziba katika kuimarisha Sanaa ya Karate Tanzania.
Sensei Magoma pia, ni mkufunzi wa Sanaa ya Yoga na anauzoefu mkubwa katika fani hiyo ambayo ilimpeleka nchi nyingi akiwa kama mwalimu na wakati huohuo kufundisha Karate. Alipata mafunzo ya Sanaa ya Yoga nchini India kutoka katika chuo cha “Neo-Humanist Studies” katika mji wa Varanasi, India mwaka 1983.
Mengi aliyafanya akiwa bado nchini kwa wakati huo, ni pamoja na kutenganisha darasa la mafunzo ya Karate la watoto na watu wazima na kuliita kwa jina ka heshima ya mwanzilishi wa shule hiyo “ Bomani Brigade” au “BB” kama ilivyokuwa anavyoitwa. Kundi hilo la vijana wagodo, lilikuwa halisomi Karate tu, bali pia mwalimu Magoma alijitolea muda wake wote kuwasaidia kimasomo yao kama vile kuwafundisha “Tuition” ya hisabati, Kiingereza, na kuandika isha mbalimbali zinazohusu maisha kiujumla. Leo hii, ni Zaidi ya miaka takriban therasini na Zaidi wale vijana wamefaidika sana kwa mfano kuna wengi wao kwa hivi sasa ni walimu wa Sanaa ya Karate pia.
Sensei Magoma, ni mwalimu mwenye upeo wa hali ya juu sana katika Sanaa ya Karate ya Okinawa Goju Ryu Karate-do Jundokan Kyokai na kama nilivyoeleza hapo awali, amewacha pengo kubwa mno ambalo sasa ni zahiri kwamba kurejea kwake katika kufundisha sanaa hii nchini, kunaweza kuwahamasisha walimu wengi na kuiga mfano wake wa kuwa na moyo na nia ya kusaidia vijana na kuwapa nidhani katika maisha yao ya baadae.
Kwa mengine Zaidi yanayohusika na Sensei Magoma na jinsi yakuwasiliana nae yatafuatia hao baadae.
No comments:
Post a Comment