Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akiongea na wajumbe mbalimbali waliofika katika uzinduzi wa kivuko cha kigamboni jana jijini Dar es Salaam kinachofanyiwa matenganezo na Jeshi la Wanamaji maeneo ya kurasini, ambacho kinatarajiwa kuanza kutumika rasmi alhamisi wiki hii.
Mtendaji Mkuu Temesa Injinia Marceline Magesa akitoa neno la shukrani kwa Jeshi la Wanamaji waliwezesha matengenezo ya Mv Kigamboni jana jijini Dar es Salaam ambapo kinatarajiwa kuanza kutumiwa na wananchi wiki hii.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli ( kushoto) na Katibu Mkuu wa Ujenzi Injinia Mussa Iyombe(kulia) wakisikiliza kwa makini maelekezo yaliyokuwa yakitolewa katika ufunguzi wa kivuko cha Mv Kigamboni jana jijini Dar es Salaam kinachofanyiwa matenganezo na Jeshi la Wanamaji maeneo ya kurasini na kinatarajiwa kuanza kutumika wiki hii.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli ( katikati) akipata maelekezo kutoka kwa Msimamizi wa matengenezo Luten Kanali Abel Gwanafyo (Kushoto), kulia ni Mkuu wa Jeshi la Maji Brigadia Jenerali Rostian Laswai wakati wa ufunguzi wa kivuko hicho jana jijini Dar es Salaam ,amabapo kinatarajiwa kuanza kutumika wiki hii kurahisisha usafiri kwa watu wa Kigamboni.
Kivuko cha Mv Kigamboni kinavyoonekana kwa ndani, kinatarajiwa kuanza kutumika siku ya alhamisi baada ya matengenezo yaliyofanywa na Jeshi la Wanamaji kwa mda wa wiki tatu tangu kilipoacha kufanya kazi Agosti 14 mwaka huu.
Kivuko cha Mv Kigamboni kinavyoonekana upande wa mbele na ubavuni , kikiwa katika hatua za mwisho tayari kwa kuanza kutumiwa na wananchi siku ya alhamisi baada ya matengenezo yaliyofanywa na Jeshi la Wanamaji kwa mda wa wiki tatu tangu kilipoacha kufanya kazi Agosti 14 mwaka huu.( Picha na Lorietha Laurenc eMaelezo).
No comments:
Post a Comment