ANGALIA LIVE NEWS

Monday, October 20, 2014

Boko Haram wafanya mashambulizi

Watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa Boko Haram, wamewapiga risasi na kuwachinja watu katika vijiji vitatu Kaskazini Mashariki ya Nigeria licha ya serikali kudai mwishoni mwa wiki kuwa ilifikia makubaliano na kundi hilo.

Wapiganaji wa Boko Haram, walivamia vijiji viwili Jumamosi na kupandisha bendera yao kwa mara ya tatu. Hii ni kwa mujibu wa wanakijiji wa eneo hilo.

Serikali ilisema kuwa itaendelea kufanya mazungumzo na Boko Haram licha ya madai ya kundi hilo kuvunja makubaliano.

Inatumai kuwa kundi hilo litawaachilia zaidi ya wasichana miambili waliowateka nyara amwezi Aprili.

Boko Haram hawajasema chochote kuhusu tamko la serikali ya Nigeria Ijumaa kwamba wamekubali kusitisha vita na kuwaachilia wanafunzi hao miambaili waliotekwa nyara katika eneo la Chibok.

'ahadi yatimizwa'

Inaarifiwa Boko Haram wanawakilishwa kwenye mazungumzo ya upatanishi yanayofanyika nchini Chad na Danladi Ahmadu. .

Hata hivyo, duru zinsema mwakilishi wa kundi hilo ni mtu bandia asiyetambulika na Boko Haram.

Hatua ya serikali kukosa kuwaokoa wasichana hao imesababisha maandamano nchini Nigeria. Wasichana hao walipotekwa nyara dunia nzima ilishtuka na hata kuanzisha kampeini ya kutaka serikali kuwaokoa wasichana hao.

Mpatanishi mkuu wa serikali Hassan Tukur amesema kuwa kundi hilo lilitimza ahadi yake ya kwanza kwa kuwaachilia raia 27 wa Cameroon na wachina, tarehe 11 Oktoba baada ya kuwateka nyara mwezi Mei na Julai.

"kwa kuwa wapiganaji hawa walitimiza ahadi yao ya kuwaachilia raia wa Cameroon tuna matumaini kuwa watawaachilia wasichana hao wa Chibok pamoja na kusitisha vita.''

BBC

No comments: