ANGALIA LIVE NEWS

Monday, October 20, 2014

FILAMU YA DOGO MASAI YASHINDA TUZO MAREKANI

Na Myovela Mfwaisa TCA.
FILAMU  ya kitanzania ya Dogo Masai iliyotengenezwa na kuongozwa na muongozaji Timoth Conrad ‘Tico’ imeibuka kidedea baada ya kushinda katika tuzo za Silcon Valley African Film Festival (SVAFF) kama Filamu Bora kutengenezwa Afrika (The best African Production Movie ) tuzo hizi zimetolewa California Marekani.

Mtayarishaji wa filamu hiyo Timoth kupitia kampuni yake ya Timamu African Media amesema ushindi huo ni wa Tanzania ndio maana hata kama hakupewa Support na taasisi yoyote kutoka Serikalini lakini amefurahia kulitangaza Taifa kwa juhudi zake binafsi.

“Nimepokelewa hapa California kama mfalme kwa ajili ya kuwania tuzo kubwa na yenye thamani kubwa, hapa nimeongelea fahari ya Taifa langu Tanzania, ni ushindi mkubwa sana nimepeperusha Bendera ya Tanzania,”

“Ninayo furaha kubwa sana kushinda tuzo hii kupitia filamu yangu ya Dogo Masai, tuzo hii kwangu ni ya pili, baada ya tuzo ya Mdundiko kushinda, na tumeona ni bora kutumia gharama kutafuta tuzo kubwa kwetu hatuna tuzo,”anasema Tico.

Filamu ya Dogo Masai imeshinda baada ya kuzibwaga sinema kutoka  South Africa, Malawi, Egypt,  Nigeria, pamoja na Uganda. Ni ushindi wa Afrika Mashariki kwani ilikuwa ni Tanzania na Uganda ndio walifanikiwa kuingia katika tuzo hizo kubwa, bado kuna sababu ya kujivunia kama ushindi wa kishindo.

Changamoto kubwa ni kwa Basata ambao inasemekana wamekuwa wakizuia watayarishaji wasiandae kwa sababu zao ambazo hazijengi tasnia zaidi ya kudumaza, leo mtanzania anakwenda Marekani na kuibuka mshindi akitangaza Bendera ya Tanzania.

Ushindi wa filamu ya Dogo Masai ni ushindi mkubwa kwa Tanzania ni kitu cha kujivuania na iwe njia kwa watayarishaji wengine kushiriki katika tuzo mbalimbali za filamu hata Oscar, huu ni mwanzo mzuri kwa kazi za Tanzania.

Tico anawashukru wasanii wote walishiriki na kufanikisha utengenezaji wa filamu ya Dogo Masai, familia yake rafiki yake Dorice, timu nzima ya Timamu Casting Agency na kila mtu aliyeshiriki kwa mawazo na ushauri na anasema kuwa milango imefunguka kwani filamu yaDogo Masai imeingia katika kugombea tuzo nyingi.

Dogo Masai pia  imechaguliwa kuingia kwenye tuzo nyingine ya Rome Independent Film Festival (RIFF) za nchini Italy, na tayari kuna dalali za kuibuka na ushindi kwani watengenezaji wa filamu wamekuwa wakiiongelea katika mitandao mbalimbali, tuzo hizo zinatarajiwa kufanyika mwakani mwezi wan ne Dogo Masai ni balozi kuitangaza Tanzania.

No comments: