ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, October 12, 2014

CCM NEW YORK YAFANYA UCHAGUZI NA KUPATA VIONGOZI WAO WA TAWI

Mwenyekiti wa tume huru ya uchaguzi Bwana Isaac Kibodya akitoa maelezo ya jinsi ya upigaji kura. Tawi la CCM New York lilifuguliwa Miaka mitatu iliyopita lilikuwa alijawahi kufanya uchaguzi na kipindi hicho chote lilikuwa linaongozwa na viongozi wa muda. Sasa Tawi limepata viongozi wake Mwenyekiti ni Seif Akida na viongozi wengi ni katibu mwenezi wa siasa ni Steve Bubelwa, wajumbe ni bwana Magawa Ernest, Mauris Mwingira, Shaban Mseba na Ibrahim Selungwi. Kwa upande wa umoja wa vijana waliochaguliwa na Gaston Mkapa na Bahia Maundi mweka hazina ni Sophia Yona. Pongezi ziwaendee kamati ya uchaguzi iliyokuwa inaongozwa na Bwana Isaac Kibodya, Joyce Mkapa, Hamisa Maundi na Justin na kusimamiwa na Loveness Iron Lady kutoka Washington. DC 
Balozi Tuvako Manongi akiwapongeza viongozi wapya waliyochagulia katikati ni mwenyekiti wa uchaguzi bwana Kibodya na kushoto ni Loveness akimsikiliza balozi. 
Ukodak wa pamoja wajumbe na viongozi wapya wa tawi la CCM New York baada ya uchaguzi huo. 

No comments: