Advertisements

Tuesday, October 21, 2014

DIAMOND MATATANI KWA KUPANDA JUKWAA LA FIESTA NA MAVAZI YA JWTZ

UFUATIA picha zilizoenea katika mitandao ya Kijamii, kuhusiana na msanii huyo kutinga mavazi hayo, hivi sasa Jeshi la Polisi limemfungulia mashitaka msanii huyo kwa tuhuma za kupanda jukwaani akiwa na sare za jeshi.

Katika Onyesho hilo lililofanyika kwenye Viwanja vya Leaders Club Kinondoni, mwishoni mwa wiki iliyopita, pia wasanii kadhaa akiwapo Ney wa Mitego pia walipanda jukwaani na wanenguaji wao wakiwa wametinga mavazi kama hayo aliyotinga Diamond.

Kutokana na tukio hilo, Kamanda wa Polisi Wilaya ya Kinondoni, C. Wambura, alisema kuwa tayari ameshafungua Jalada la uchunguzi kuhusu msanii huyo kumiliki mavazi hayo na kuongeza kuwa baada ya uchunguzi kukamilika hatua zitafuata ikiwa ni pamoja na kumtia mbaroni msanii huyo na kumpandisha mahakamani ili kujibu tuhuma hizo.

Aidha alisema kuwa hivi sasa bado msanii huyo anafanyiwa uchunguzi kubaini kuwa mavazi hayo aliyapata wapi na baada ya kukamilika kwa uchunguzi atachukuliwa hatua.

2 comments:

Anonymous said...

Ovyo makosa hamyaoni yanayofanyika tz eti magwandwa so what

Anonymous said...

Hivi hawa wanajeshi hawana vitu vingine muhimu vya kufanya?