ANGALIA LIVE NEWS

Monday, October 6, 2014

HALI YA MBUNGE WA UKAWA HIGHNESS KIWIA NI MBAYA

HALI ya Mbunge wa Ilemela, Highness Kiwia (CHADEMA), imeelezwa kuwa mbaya kutokana na kushindwa kupumua kwa kutumia pua na badala yake anatumia mdomo kitendo ambacho ni hatari.
Taarifa hiyo imetolewa jana na Kiongozi wa Operesheni Kanda ya Ziwa Magharibi, Tungaraza Njugu, wakati Baraza la Vijana CHADEMA (BAVICHA), wakitoa tamko juu ya Polisi kwa kushirikiana na Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuhatarisha amani ya nchi.
Kiwia, alisafirishwa kwenda India usiku wa Septemba 28 mwaka huu,
kwa ajili ya uchunguzi zaidi na matibabu ya afya yake kutokana na matatizo ya mishipa ya kichwa.
Mbunge Kiwia, alikumbwa na tatizo hilo baada ya kushambuliwa kwa mapanga na watu wanaosadikika kuwa ni wafuasi wa CCM katika uchaguzi mdogo wa udiwani Kata ya Kirumba jijini hapa

No comments: