Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akisaini katika Kitabu cha Maombolezo nyumbani kwa aliyekuwa Afisa Mnadhimu Mkuu Msaidizi wa Jeshi la Magereza, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Stephen Nzawila ambaye amefariki Jumapili tarehe 19 Oktoba, 2014 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam.
Mwili wa aliyekuwa Afisa Mnadhimu Mkuu Msaidizi wa Jeshi la Magereza, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Stephen Nzawila ukiwa umebebwa na Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza kabla ya kuagwa rasmi leo Oktoba 20, 2014 nyumbani kwake, Ukonga Dar es Salaam.
Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(suti nyeusi) akiwa amesimama wakati mwili wa aliyekuwa Afisa Mnadhimu Mkuu Msaidizi wa Jeshi la Magereza, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Stephen Nzawila ulipowasili tayari kwa kuuagwa rasmi nyumbani kwake Ukonga, Dar es Salaam leo Oktoba 20, 2014(wa kwanza kushoto) ni Kamishna Mkuu Mstaafu wa Magereza, Nicas Banzi(wa pili kushoto) ni Kamishna Mkuu Mstaafu wa Magereza, Jumanne Mangara(wa kwanza kulia) ni Kamishna wa Fedha na Utawala, Gaston Sanga(wa pili kulia) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa.
Mchungaji wa Kanisa la Moravian lililopo Ukonga, Banana Relini Hansi Mwakijoja akiwaongoza Waombolezaji kwa sala kabla ya kuuaga rasmi mwili wa aliyekuwa Afisa Mnadhimu Mkuu Msaidizi wa Jeshi la Magereza ambaye amefariki Jumapili Oktoba 19, 2014 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akitoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Afisa Mnadhimu Mkuu Msaidizi wa Jeshi la Magereza ambaye amefariki Jumapili Oktoba 19, 2014 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam.
Baadhi ya Maofisa na Askari wa Jeshi la Magereza wakiwa wamejipanga katika mstari tayari kuuaga mwili wa aliyekuwa Afisa Mnadhimu Mkuu Msaidizi wa Jeshi la Magereza leo Oktoba 20, 2014 Ukonga, Jijini Dar es Salaam. Mwili wa Marehemu unatajiwa kusafirishwa kesho kuelekea Tutuo Wilayani Sikonge, Mkoani Tabora kwa Mazishi.
Mke wa Aliyekuwa Afisa Mnadhimu Mkuu Msaidizi wa Jeshi la Magereza akiwa na majonzi makubwa na waombolezaji kabla ya kuuaga rasmi mwili wa mume wake ambaye amefariki Jumapili Oktoba 19, 2014 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam.
Sehemu ya Waombolezaji waliojitokeza kuuaga mwili wa aliyekuwa Afisa Mnadhimu Mkuu Msaidizi wa Jeshi la Magereza wakisikiliza kwa makini wasifu wa Marehemu kabla ya kuuaga rasmi leo Oktoba 20, 2014 Ukonga, Dar es Salaam.
Bendi ya Jeshi la Magereza ikitumbuiza katika hafla fupi ya kuuaga mwili wa aliyekuwa Afisa Mnadhimu Mkuu Msaidizi wa Jeshi la Magereza, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Stephen Nzawila ambaye amefariki Jumapili Oktoba 19, 2014 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).
No comments:
Post a Comment