Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu Tuzo iliyotolewa na Rais Mugabe kwa Brig. Jen. Hashim Mbita wakati wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa SADC uliofanyika Victoria Falls nchini Zimbabwe mwezi Agosti 2014. Waziri Membe alieleza kuwa Rais Mugabe alitoa Tuzo ya Munhumutapa kwa Brig. Jen Hashim Mbita kutokana na mchango wake mkubwa katika harakati za kutafuta uhuru Kusini mwa Afrika. Brig. Jen. Mbita anakuwa mtu wa kwanza sio Mkuu wa Nchi kutunukiwa Tuzo hiyo ambayo kwa kawaida hutukiwa Wakuu wa Nchi pekee. Wengine katika picha ni Balozi wa Zimbawe nchini Tanzania na binti yake Brig. Jen. Mbita, Bibi Shella.
Bibi Shella akitoa neno la shukrani kwa Serikali ya Zimbabwe kutokana na zawadi ya Dola 100,000.00 kwa Baba yake mzazi
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Shiyo Innocent (tai nyekundu) na Afisa wa Ubalozi wa Zimbabwe nchini Tanzania wakifuatilia kwa makini mkutano wa waandishi wa habari
Waandishi wa habari wakiwa kazini.
1 comment:
Wakati nasoma Chang'ombe primary Dar huyu mzee Mbita alikuwa anawika sana kwenye redio kuhusiana na ukombozi wa nchi za Afrika, kwani marehemu Raisi Nyerere alikuwa namtuma huko.
Sasa kama yeye ni mtumishi wa serikali inakuwaje pesa apewe yeye??
Hizo pesa zingeenda kwenye mfuko wa kusaidia elimu au kununua mashine za kuchunguza ugongwa wa EBOLA.
Jamani kwa nini serikali inaruhusu mambo mengi kama ubinafsi kama huu??
Hebu tuseme kama ingekuwa nchi nyingine hii ingekubalika kweli??
NAOMBA KUELIMISHWA WATANZANIA WENZAGU>
Post a Comment